Aprili 06, 2017, Dar es Salaam, Tanzania
Benki ya Barclays Tanzania leo imezindua huduma ya
Union Pay kama njia moja wapo ya kuwarahisishia wateja wenye kadi za Union Pay
kufanya miamala na kutumia kadi zao wakiwa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji, Abdi Mohamed amesema benki ya
Barclays Tanzania imezindua huduma hii ambayo itatolewa kupitia mashine za ATM
na POs zilizosambaa nchini.
Huduma hii ni nafasi kubwa kwa wafanya biashara
wenye POs kwenye maduka, hoteli, migahawa, mbugani na kadhalika kuweza
kuwahudumia na kufanya biashara wateja wenye kadi za Union Pay .
“Huduma ya Union Pay
inapatikana nchi 160 duniani ambazo zinaongoza kwa kutembelewa na wachina kwa
ajili ya biashara, kazi au starehe ikiwamo Tanzania hivyo tumeona fursa na haja
ya kuanzisha huduma hii kwa wateja wenye kadi za Union Pay kupitia mashine zetu
za ATM na POs.
Kwa mzunguko wa zaidi ya
POs 500 na ATM 52 nchini, huduma hii itawasaidia wateja kwa kukidhi mahitaji
yao kwa wakati na kama mpango mkuu kwa benki tutahakikisha inawafaidisha
watumiaji wa Union Pay nchini na dunia nzima” alisema Abdi.
Union Pay International inayojulikana kama Union Pay ni huduma kuu ya
kifedha inayopatikana kupitia kadi za kibenki na ina makao makuu yake mjini
Shanghai, China.
Huduma hii imezinduliwa Machi 26, 2002 na inaendeshwa chini ya benki kuu
ya China - People’s Bank of China (PBOC)
Mkuu wa Maendeleo ya Biashara wa Kadi ya Union Pay, Herman Botes
(kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya kadi ya China Union Pay
ya Benki ya Barclays Tanzania kama njia moja wapo ya kuwarahisishia wateja wenye
kadi hizo kufanya miamala na kutumia kadi zao wakiwa nchini kupitia benki hiyo.
Uzinduzi umefanyika jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto kwake ni Mwakilishi
wa Ubalozi wa China, Gao Wei, Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Abdi
Mohamed, Mkurugenzi wa Huduma Rejareja na Biashara wa Barclays, Kumaran Parther
na Meneja wa Kadi wa benki hiyo, Philbert Casmir.
Mwakilishi wa Ubalozi wa China, Gao Wei akizungumza wakati wa uzinduzi
wa huduma ya kadi ya China Union Pay ya Benki ya Barclays Tanzania kama njia
moja wapo ya kuwarahisishia wateja wenye kadi hizo kufanya miamala na kutumia
kadi zao wakiwa nchini kupitia benki hiyo. Uzinduzi umefanyika jijini Dar es
Salaam. Wengine kushoto kwake ni, Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania,
Abdi Mohamed, Mkurugenzi wa Huduma Rejareja na Biashara wa Barclays, Kumaran
Parther.
Mkurugenzi wa Huduma Rejareja na Biashara wa Barclays, Kumaran Parther akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma ya kadi ya China Union Pay.
Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Abdi Mohamed, akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma ya kadi ya China Union Pay ya Benki ya Barclays
Tanzania kama njia moja wapo ya kuwarahisishia wateja wenye kadi hizo kufanya
miamala na kutumia kadi zao wakiwa nchini kupitia benki hiyo. Uzinduzi umefanyika
jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Ubalozi wa China, Gao Wei,
kulia ni Mkurugenzi wa Huduma Rejareja na Biashara wa Barclays, Kumaran Parther
na Meneja wa Kadi wa benki hiyo, Philbert Casmir.
Mwakilishi wa Ubalozi wa China, Gao Wei, akizungumza wakati wa uzinduzi
wa huduma ya kadi ya China Union Pay ya Benki ya Barclays Tanzania kama njia
moja wapo ya kuwarahisishia wateja wenye kadi hizo kufanya miamala na kutumia
kadi zao wakiwa nchini kupitia benki hiyo. Uzinduzi umefanyika jijini Dar es
Salaam. Wengine kushoto kwake ni Mkuu wa Maendeleo ya Biashara wa Kadi ya Union
Pay, Herman Botes na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Abdi
Mohamed.
Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Abdi Mohamed akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kadi ya China Union Pay ya
Benki hiyo.
Meneja wa Kadi wa benki hiyo, Philbert Casmir, akizungumza na waandishi
wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kadi ya China Union Pay ya Benki
hiyo.
Meneja wa Kadi wa benki hiyo, Philbert Casmir, akitoa maelekezo jinsi ya
kutumia mashine ya Pos maalumu
yenye kuruhusu huduma ya kadi ya China Union Pay ya Benki hiyo.
ATM maalumu zenye kuruhusu huduma ya kadi ya China Union Pay ya Benki
hiyo.
Meneja wa Kadi wa benki hiyo, Philbert Casmir, akitoa maelekezo jinsi ya
kutumia ATM maalumu zenye uwezo wa kuruhusu huduma ya kadi ya China Union Pay
ya Benki hiyo.
Mwakilishi wa Ubalozi wa China, Gao Wei, Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays
Tanzania, Abdi Mohamed, Mkurugenzi wa Huduma Rejareja na Biashara wa Barclays, Kumaran
Parther kwenye picha ya pamoja.
Afisa wa Benki ya Barclays akitoa maelekezo jinsi ya kuitumia mashine ya
Pos maalumu yenye kuruhusu huduma ya kadi ya China
Union Pay ya Benki hiyo.
Mkuu wa Maendeleo ya Biashara wa Kadi ya Union Pay, Herman Botes, akiteta
jambo na Mwakilishi wa Ubalozi wa China, Gao Wei, na Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays
Tanzania, Abdi Mohamed.
No comments:
Post a Comment