Mmoja wa wanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Elias Makala (wa tatu kushoto),
ambaye yeye na wenzake wawili, Elead Mrina (kushoto) na Samwel Sirikwa
kupitia kampuni yao ya TanzDevs Co waliibuka washindi wa mradi wa
shindano la wanafunzi wajasiriamali lililodhaminiwa na Benki ya Barclays
Tanzania, wakiwa katika mkutano wao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana. Elias ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya wanafunzi
wajasiriamali yanayotarajiwa kufanyika nchini Ujerumani hivi karibuni.
Wanaoangalia kutoka kulia Mwanzilishi wa University Entrepreneurship
Challenge, Victor Joseph na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Barclays Tanzania,
Aron Luhanga.
Mmoja wa wanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Elias Makala (katikati), ambaye yeye
na wenzake wawili, Samwel Sirikwa (kushoto) na Elead Mrina (hayupo pichani)
kupitia kampuni yao ya TanzDevs Co waliibuka washindi wa mradi wa
shindano la wanafunzi wajasiriamali lililodhaminiwa na Benki ya Barclays
Tanzania, wakionyesha moja ya ubunifu wao wa kutumia teknolojia ya 3D katika
kusoma vitabu wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana. Elias ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya wanafunzi
wajasiriamali yanayotarajiwa kufanyika nchini Ujerumani hivi karibuni.
Anayeangalia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Barclays Tanzania, Aron
Luhanga.
Mkuu wa Masoko na
Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (wa pili kulia),
akizungumza jjini Dar es Salaam jana wakati wakitangaza washindi wa mradi wa
shindano la wanafunzi wajasiriamali lililodhaminiwa na benki hiyo ambapo
wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kupitia kampuni yao ya
TanzDevs Co waliibuka kidedea. Elias ataiwakilisha Tanzania katika mashindano
ya kimataifa ya wanafunzi wajasiriamali yanayotarajiwa kufanyika nchini
Ujerumani hivi karibuni. Pichani kutoka kushoto ni wanafunzi hao, Elead Mrina,
Samwel Sirikwa na Elias Makala wa UDSM, na kulia ni Mwanzilishi wa
University Entrepreneurship Challenge, Victor Joseph.
Mwanzilishi wa University Entrepreneurship Challenge,
Victor Joseph akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa kumtangaza
mshindi mradi wa shindano la wanafunzi wajasiriamali lililodhaminiwa
na benki hiyo ambapo wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
kupitia kampuni yao ya TanzDevs Co waliibuka kidedea. Mmoja wa wanafunzi hao, Elias
ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya wanafunzi
wajasiriamali yanayotarajiwa kufanyika nchini Ujerumani hivi karibuni. Kushoto
kwake ni Mkuu Kitengo cha Masoko na
Mahusiano Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga, pamona na washindi hao.
Benki ya Barclays Tanzania Limited kupitia mfumo wake
wa huduma za jamii inawezesha makampuni kuimarisha maendeleo ya jamii na
kujikwamua kiuchumi kupitia masoko na vitendea kazi. Mfumo endelevu wa jamii ni zaidi ya misaada
tu kwa jamii kwa sababu inalenga kupata faida inayokuza biashara na jamii kwa
ujumla.
Vijana wengi nchini wamekosa ufanisi wa kuendeleza
biashara zao na kuimarisha ukuaji wa uchumi na kipato chao kutokana na mfumo
duni nchini ambao hauwapi fursa ya maendeleo. Hii inaashiria upotevu mkubwa wa
nguvu kazi nchini na inapelekea ongezeko la uhalifu na maisha duni kwa vijana.
Benki ya Barclays Tanzania limited kwa kushirikiana
Mashindano ya Wanafunzi Wajasiriamali inalenga kuleta mabadiliko katika jamii
kw alengo la kukuza na kuimarisha ushumi na biashara kw aujumla.
Mashindano ya Wanafunzi Wajasiriamali
ni mradi unaolenga kuwatambua na kuwasaidia vijana waliopo vyuoni kuanzisha na
kuendeleza biashara zao kwa maendeleo ya uchumi wao binafsi nan chi kwa ujumla.
Mradi huu unasisitiza katika ubunifu na hari ya kujenga utamaduni w akujiajiri
zaidi kwa wanafunzi waliopo vyuoni, asema Victor Joseph ambaye ndiye
muanzilishi wa mashindano hayo.
Mshiriki huyu aitwaye Elias Elisante ni
mmiliki wa kampuni iitwayo TanzDevs Co, ambayo imeundwa na wanafunzi watatu
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wanatengeneza vifaa vya kusomea na
kuwasilisha elimu kwa njia rahisi. Vifaa hivi vimeundwa kumuwezesha na kumsaidia
msomaji kuona kwa video na kuelewa kwa sauti ya maelezo ya kilichoandikwa kupitia
teknohama iitwayo 3D.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mahusiano
wa Benki ya Barclays Tanzania , Aron Luhanga asema, “Maendeleo ya Ujasiriamali
ni kipaumbele katika huduma zetu za jamii na ni muhimu kwetu kusaidia katika
kuwezesha uchumi wa nchi yetu na kuwapa vijana kipaumbele katika kujenga na
kuwezesha biashara zao ambazo zinapunguza ukosefu wa ajira na kutoa ajira kwa
vijana wenzao”.
Mashindano haya ya Wanafunzi duniani
yanawafanya wanafunzi duniani kukutana na kuonesha ubora wa biashara zao kwenye
ujasiriamali na ilianzishwa mwaka 1998 na Chuo cha Mtakatifu Luisi ambayo kwa
sasa inajumuisha program ya mashirika mbali mbali ya wajasiriamali.
TanzDevs
Co. watashindana na wanafunzi wengine duniani kwa lengo la kusaidia wanafunzi
wajasiriamali ambao wanahitaji mafunzo na kutambulika katika biashara zao na
kujiendeleza kibiashara.
No comments:
Post a Comment