Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Wenye ulemavu,
Jenista Mhagama amewaasa Watanzania kuwa wazalendo pamoja na kudumisha amani na
utulivu uliopo nchini.
Akizungumza,
leo mjini Dodoma wakati akifuatatilia maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya
Muungano yatakayofanyika Aprili 26 mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri uliopo
mjini Dodoma.
“Tunapoadhimisha
miaka 53 ya Muungano ninawaomba watanzania kuwa wazalendo pamoja na kulinda
amani ya nchi” alisema Waziri Mhagama
Pia, Waziri
Mhagama aliwaomba watanzania hasa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi katika
Maadhimisho hayo yatakayofanyika jumatano wiki hii.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema kuwa mkoa wake
umejipanga vizuri katika kufanikisha maadhimisho hayo, ambapo pia alivishukuru
vyombo vya habari kwa kuhamasisha wananchi juu ya maadhimisho hayo.
“Wananchi
wamehamasika kushiriki katika maadhimisho haya ya miaka 53 ya Muungano, ninawashukuru
kwa kazi kubwa mliyoifanya na tunaamini mtaendelea kuhamasisha wananchi
kushiriki katika maadhimisho hayo” alisema Rugimbana
Maandalizi ya
Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya
Dodoma mjini Christina Mndeme, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Aidha, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ambapo pia yatahudhuriwa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein na
viongozi mbalimbali wa dini na Serikali.
Maadhimisho
hayo ya miaka 53 ya Muungano yanatarajiwa kupambwa namaonesho kutoka kutoka
vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama, burudani za vikundi vya ngoma pamoja
na maonesho ya halaiki.
Waziri Mhagama akikagua maandalizi ya kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya
Muungano katika viwanja vya Jamhuri leo Mjini Dodoma.
Baadhi ya wananchi
wakifuatilia maonesho ya maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma
kwa mara ya kwanza tangu Serikali ilipohamia Dodoma.
Vikosi vya Ulinzi na
Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya
miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe
26 Aprili Mjini Dodoma.
Vikosi vya Ulinzi na
Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya
miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe
26 Aprili Mjini Dodoma.
Vikosi vya Ulinzi na
Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya maadhimisho ya Maadhimisho ya
miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe
26 Aprili Mjini Dodoma.
Askari wa Pikikipi
maalum wakionesha namna pikipiki hizo zitakavyopamba maonesho hayo.
Makomandoo wa Jeshi
la wananchi wa Tanzania wakionesha umahiri wao wa kuvuta gari lenye tani 7
ikiwa ni moja ya mbinu ya medani katika uwanja wa mapambano.
Askari wa Kikosi cha
Farasi wakionesha umahiri wao katika kutumia farasi kupambana na uhalifu.
Wanafunzi wa halaiki
wakipita kwa ukakamavu mbele ya Jukwaa Kuu.
No comments:
Post a Comment