Shirika la Anga la Etihad
limetangaza uteuzi wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Idara yake tanzu ya Airline Equity
partners, Bwana Robin Kamark ambaye atashughulikia kuongoza na kuendeleza
mikakati ya uwekezaji inayojumuisha wabia wa Shirika hilo kama vile; Airberlin,
Alitalia, Jet Airways, Air Serbia, Air Seychelles, Etihad Regional na Virgin
Australia.
Mtendaji huyo mkuu
atakuwa chini ya Rais wa Shirika hilo na Mkurugenzi Mkuu. Kamark anachukua
nafasi ya Bruno Matheu ambaye alishika wadhifa huo tangu Mei 2016 ambaye
imeelezwa kwamba anaachia ngazi kutokana na sababu zake binafsi.
Kamark amefanya kazi
katika sekta ya anga kwa takriban miaka 17, huku akifanikiwa kufikia malengo ya
mikakati yake ya kibiashara na masuala ya utawala katika Shirika la SAS ambako
pia alikuwa akitekeleza majukumu yake kama Ofisa Mkuu wa Biashara.
Kwa miaka mitano yake ya
mwishoni amefanya kazi kama Makamu wa Rais na Ofisa Mkuu wa Biashara katika
kitengo cha bidhaa za ASA zinazoongoza kwa huduma za kifedha na biashara.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Shirika la Anga la Etihad, Mhe. Mohamed Mubarak Fadhel Al Mazrouei amesema
kwamba “Shirika hili linaendelea kuwekeza duniani katika kiwango chenye ubora
wa juu, ikiwamo kujenga timu nzuri itakayoongoza biashara na kuipelekea katika hatua
kubwa zaidi za maendeleo.”
Alisema, “Robin ni
kiongozi anayeheshimika katika sekta ya anga duniani pia ana uzoefu mkubwa
kutoka Shirika la SAS. Amefanya kazi kubwa ya kuboresha shirika hilo la ndege.
Hivi karibuni amepanua wigo wa taaluma yake katika masuala ya huduma za
kifedha.”
Aliongeza kuwa,
“Ushirikiano na kampuni yetu utaendelea kuwa alama muhimu katika biashara na
Robin ataongoza mipango hiyo kwa kuweka mikakati na kuendeleza dhamira yetu.”
“Tunapenda kumshukuru
Bruno kwa juhudi zake kubwa alizoonyesha kwa kipindi cha miaka miwili na nusu
kutokana na kufanikiwa kujenga na kuhimarisha ushirikiano wetu katika kitengo
cha Airline Equity partners,” alisema kiongozi huyo.
Kamark ataongoza mikakati
ya maendeleo kwa kuongeza ufanisi katika biashara, mapato na kuboresha bei
baina ya Shirika la Ndege la Etihad na wabia wake ulimwenguni. Pia atasimamia
mikakati ya kiutawala kwa wabia wa mashirika ya ndege ambayo Shirika la Etihad
linashirikiana nayo.
Kamark amepata elimu ya
shahada ya kwanza na uzamili katika masula ya uongozi wa biashara, huku akifuzu
kwenye Shule ya Utawala ya Norwegian.Alianza kazi ya uhasibu katika sekta ya
viwanda vya uzalishaji bidhaa, pia alitumikia jeshi kabla ya kujiunga na SAS
mwaka 1995.Kamark ataanza majukumu yake rasmi Oktoba mwaka huu.
Akishukuru uteuzi huo
Kamark alisema, “Ninaishukuru Bodi ya Shirika la Anga la Etihad kwa ujasiri wao
wa kuniteua. Haya ni majukumu makubwa, kunipa nafasi hii muhimu kuendeleza na
kuboresha mikakati muhimu ya Shirika.”
Ofisa Mikakati na Mipango
wa Shirika hilo, Kevin Knight ataungana na Bruno Mathew katika kuendeleza Idara
ya Airline Equity Partners.
Kamark anakuwa miongoni
mwa watendaji wa juu katika Shirika la Anga la Etihad akiungana na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad (Peter Baungartner), Mkurugenzi wa Kitengo
cha Uhandisi cha Shirika la Ndege Etihad (Jeff Wilkinson), Mkurugenzi Mtendaji
wa Huduma za Uwanja wa Ndege (Chris Youlten).
Uongozi wa Shirika la
Hala linalohusika na masula ya Masoko na Huduma za Hadhi ya juu, watatangaza
mkurugenzi wake wa kudumu mwishoni mwa mwaka huu.
Bodi ya Shirika la EAG
kwa sasa linaendelea na mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu wake mpya ambaye
atachukua nafasi ya Rais na Mkurugenzi wa sasa, James Hogan ambaye awali
ilitangazwa ataachia ngazi baadaye mwaka huu.
No comments:
Post a Comment