BENKI YA KCB TANZANIA YADHAMINI MKUTANO WA WATANZANIA WANAOISHI NJE YA NCHI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, April 28, 2017

BENKI YA KCB TANZANIA YADHAMINI MKUTANO WA WATANZANIA WANAOISHI NJE YA NCHI


Benki ya KCB Tanzania yadhamini mkutano wa Watanzania wanaoishi nchini Marekani. Mkutano huo utafanyika tarehe 5 7 Mei 2017 katika hoteli ya Wyndham Dallas Suites - Park Centrale, Dallas, Texas. Na unategemewa kuhudhuriwa na watanzania elfu moja kutoka majimbo mbalimbali ya Marekani.

Akizungumza kuhusiana na mkutano huu, Meneja Mahusiano wahuduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Shose Kombe alisema Texas ni mji wenye watanzania wengi wakiwemo wanafunzi, wafanyakazi na wafanyabiashara wenye mahitaji ya huduma za kibenki kutoka Tanzania.

Tunaelewa kuwashughuli za kutafuta kipato na elimu hupelekea watanzania wengi kuenda sehemu mbalimbali duniani na kuishi huko kwa muda mrefu na hivyo huhitaji kuwekeza na kupata huduma za kibenki nyumbani wakiwa mbali na Tanzania. Alisema Bi. Kombe.

Meneja huyo alisema kuwa Benki ya KCB inawapatia watanzania wanaoishi nje ya nchi huduma bora za kibenki ikiwemo akaunti za akiba (savings), akaunti za uwekezaji (Investment), akaunti za wanafunzi, akaunti za watoto na fursa ya kununua nyumba (Mortgage) kwa lengo la kuwawezesha watanzania hao kuendesha shughuli zao za kibenki Tanzania huku wakiwa nje ya nchi na kupata akiba zao pindi watakaporudi nchini Tanzania. 

Aliongeza kwamba huduma hizi za kibenki kwa watanzania wanaoishi nje ya nchini za papo kwa hapo (real time transactions), hivyo kuwawezesha wateja wake kufanya mambo kwa wakati na bila kadhia popote pale walipo duniani.

Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanapaswa kupata huduma za kibenki kwa haraka, usalama na bila usumbufu alisema Bi. Kombe. Na hivyo tunasema JIULIZE KWANINI uhangaike kuweka akiba na kuwekeza nyumba ni ukiwa mbali na Tanzania wakati benki ya KCB ipo?


Akamalizia kwa kuwataka watanzania wanaoishi nje ya nchi na bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo kupitia tovuti ya www.kcbbank.co.tz na kupata huduma za kibenki wakiwa nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages