China imesema kuwa ina waswasi mkubwa kuhusu mpango wa
nyuklia wa Korea Kaskazini, kufuatia mahojiano ya afisa mmoja wa taifa hilo na
BBC.
Naibu wa waziri wa mambo
ya nje wa Korea Kaskazini aliambia BBC kwamba Pyongyang itaendelea kuyafanyia
majaribio makombora yake na itarusha bomu la nyuklia ikibaini kwamba Marekani
inataka kuishambulia.
Msemaji wa wizara ya
mambo ya nje Lu Kang amesema kuwa China ilipinga vitendo ama matamshi ambayo
huenda yakasababisha hali zaidi ya wasiwasi.
Kumekuwa na matamshi ya
chuki kutoka kwa pande zote mbili katika siku za hivi karibuni.
Makamu wa rais wa
Marekani Mike Pence ambaye amekuwa akitembelea eneo hilo ameonya Korea
Kaskazini kutoijaribu Marekani na kusema kuwa wakati wa subira dhidi ya
Pyongyang umekwisha.
- Uwezo wa kijeshi wa Korea Kaskazini
- Trump apuuzilia mbali mpango wa Korea Kaskazini
- Trump asema Korea Kaskazini ni tatizo
Mwandishi wa BBC Stephen
McDonnel mjini Beijing anasema kuwa serikali ya China inaonekana kukerwa na
Korea Kaskazini ambaye mwandani wake.
''Nimeona ripoti ya hivi
karibuni," Bw. Lu alisema kuhusu mahojiano hayo ya BBC.
''China ina wasiwasi
mkubwa kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini na utengenezaji wa silaha''.
China inaunga mkono
mpango wote wa kusitisha uundaji wa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea,
kuimarisha amani na uthabiti katika rais ya Korea mbali na kuendelea kutatua
maswala tofauti kupitia mazungumzo na majadiliano.
Korea Kaskazini ilifanya
maonyesho ya gwaride la kijeshi wikendi iliopita na kujaribu kombora jingine
siku ya Jumapili ambalo Pentagon inasema lililipuka muda tu liliporushwa.
Pyongyang imesema kuwa
itafanyia majaribio makombora yake kila wiki na kuonya vita vikubwa iwapo
Marekani itaishambulia.
Iwapo Marekani inapanga
shambulio la kijeshi dhidi yetu, tutalipiza kwa shambulio la kinyuklia kwa
kutumia mbinu yetu, alisema naibu wa waziri wa maswala ya kigeni Song-ryol siku
ya Jumatatu.
Meli ya kubeba ndege za kivita ya USS Carl
Vinson (kushoto) na meli nyingine zilielekea Bahari ya Hindi
Baadaye bwana Pence
aliapa kulishinda shambulio lolote na kukabiliana na utumizi wowote wa silaha
za kisasa ambapo zile za nyuklia kwa kujibu na shambulio kubwa.
Meli ya wanamaji wa
marekani ya Carl Vinson inayobeba ndege za kijeshi pamoja na meli za kijeshi,
inaelekea katika bahari ya magharibi mwa Pasifiki kulingana na kamanda wa eneo
hilo kufuatia agizo la rais donald Trump wiki iliopita.
Imebainika kwamba wakati
agizo hilo lilipotolewa meli hiyo ilikuwa ikielekea upande tofauti.
Haijulikani iwapo hatua
hiyo ilifanywa kimakusudi, ni mabadiliko ya kimkakati ama mawasiliano mabaya
kulingana na mwandishi wa BBC nchini Korea Stephens Evans.
No comments:
Post a Comment