Mwanafunzi Samwel Malebo (16) anayesoma shule ya kimataifa ya Tanganyika
grade 10 alivyoelezea siasa ya Tanzania kwa sasa katika sanaa ya uchoraji kwa
kutumia michoro mbalimbali ya inayoelezea siasa katika nyanja tatu za
Demokrasia, Rushwa na Utawala Bora.
Katika michoro yake aliyoichora kwa ubunifu na kipaji cha hali ya juu kaielezea vizuri sana
siasa katika kidemokrasia, rushwa na Utawala bora. Akitoa maelezo kwa
wanafunzi na wadau mbalimbali waliotembelea maonyesho hayo yaliyofanyika tarehe
11/02/2017 Makumbusho ya Taifa amelezea kilchomvutia kuchora michoro hiyo kuwa
ni siasa ya Tanzania kwa sasa.
Akiongea na mwandishi alisema Kilichonivutia hadi kuchora micho ya
kisiasa ni nilipata msukumo toka nikiwa shule ya msingi kwani nilikuwa nasikia
mambo mbalimbali ya siasa lakini sikuwahi kufundishwa mambo haya, kwa sasa
nimekuwa naona hali halisi ndio maana nikavutiwa kuchora michoro na kuelezea
siasa kwa ujumla”.
Katika maonesho hayo Jumla ya michoro kumi imeonyeshwa na imetoa taswira ya kisiasa katika demokrasia, rushwa na
Utawala bora.
Ni vizuri kuwaendeleza vijana na kuwapa ushirikiano pale wanapoonyesha
wana kitu cha ziada na ubunifu mzuri alisema mmoja ya wadau ambao wametembelea
maonyesho hayo na kuyakubali.
Pia nikiongea na mama mzazi Bi. Leah Lugimbana amesema aligundua kipaji
cha mwanawe toka akiwa mdogo kwa kuwa alikuwa anapenda kucho chora hivyo aliona
kuna haja ya kukiendeleza na ndio maana anampa ushirikiano mkubwa.
Wanafunzi na watu mbalimbali walioona wamemsifia na kuelewa michoro kwa urahisi inachoelezea akiwemo mtalii wa Kimataifa ambaye ni Rais wa Shirika la Forodha Duniani Bwana Kunio Mikuriya amesema Nimefurahishwa na maonyesho ya mapambano dhidi ya rushwa katika kulijenga Taifa kwa faida ya wananchi pia ameonyeshw akustaajabishwa kwa jinsi kijana mdogo alivyoweza kuelezea kwa kutumia sanaa ya uchoraji.
Wanafunzi na watu mbalimbali walioona wamemsifia na kuelewa michoro kwa urahisi inachoelezea akiwemo mtalii wa Kimataifa ambaye ni Rais wa Shirika la Forodha Duniani Bwana Kunio Mikuriya amesema Nimefurahishwa na maonyesho ya mapambano dhidi ya rushwa katika kulijenga Taifa kwa faida ya wananchi pia ameonyeshw akustaajabishwa kwa jinsi kijana mdogo alivyoweza kuelezea kwa kutumia sanaa ya uchoraji.
Samwel Malebo akimpa
Maelezo Rais wa
Shirika la Forodha Dunia
Bwana Kunio
Mikuriya picha zake zinazoelezea mapambano
dhidi ya rushwa.
Samwel Malebo akiwaelezea wanafunzi
wa Shule ya Msingi Barabara ya Mwinyi
Picha zake alizochora
Samwel Malebo akijadilaina na wanafunzi mbalimbali Kuhusiana
na michoro yao na kujibu maswali mbalimbali
Samwel Malebo akiwa na mama yake Bi Leah Lugimbana
Katika ufunguzi wa Maonyesho yake ya picha.
Baadhi ya michoro kati ya 10 iliyopo kwenye onyesho hilo.
No comments:
Post a Comment