Maonesho ya tisa ya
Harusi Trade Fair yanatarajiwa kufanyika Mei 12 hadi 13 mwaka huu kwenye hoteli
ya Golden Tulip Oyststerbay Jiji Dar es salaam ili kuwapatia maharusi uwanja wa
kuchagua mahitaji yao yote kwa ukamilifu siku ya harusi yao.
Akizungumza na Waandishi
wa habari, Meneja Biashara Hamis Omary amesema maonesho hayo ni ya kipekee kwa
Afrika mashariki na hufanyika mara moja kwa kila mwaka.
"Tunawatangazia
jamii kwa ujumla watarajie maonesho yakuvutia kuburudisha pamoja na nyakati
rahisi kwa Bwana Harusi na Bibi Harusi kuandaa vitu vyao vya harusi, vilevile
kutakuwa na mitindo mipya mingi kutoka kwa wauzaji bora katika sekta ya harusi
kila maonesho yanavyoendelea kukua kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine
ndivyo ubora unavyoendelea kuongezeka" amesema.
Meneja Masoko
wa Kampuni ya 361 Degrees, Hamis Omar(kushoto) akizungumza na waandishi wa
habari akizungumza kuhusu maonesho ya tisa ya Harusi Trade Fair yanatarajiwa
kufanyika Mei 12 hadi 13 mwaka huu kwenye hoteli ya Golden Tulip Oyststerbay
Jiji Dar es salaam.
Kaimu Meneja
wa Hoteli ya Golden Tulip, Adele Johnson (kushoto) akizungumzia na
waandishi wa habari leo kuhusu jinsi walivyodhamini maonesho ya tisa ya Harusi
Trade Fair yanayotarajiwa kufanyika Mei 12 hadi 13.
Mratibu wa
matukio wa Kampuni ya 361 Degrees, Naomi Godwin akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu mafanikio waliyoyapata kwenye maonesho yaliyopita.
Mmoja wa
waandishi wa habari akiuliza swali kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa
Maelezo jijini Dar leo.
No comments:
Post a Comment