Mshindi wa Sh Milioni 10 wa mchezo wa kubahatisha
wa Biko, Christopher Mgaya, akipokea fedha zake alizoshinda baada ya kutangazwa
mwishoni mwa wiki na kukabidhiwa mapema jana Makao Makuu ya NMB jijini Dar es
Salaam sambamba na kupewa elimu ya kifedha ili fedha hizo zimnufaishe kiuchumi
na kubadilisha maisha yake. Kulia kwake ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope
Heaven.
Ofisa wa Benki ya NMB kushoto akimkabidhi kadi yake
ya benki mshindi wa shindano la bahati nasibu ya Biko baada ya kushinda Sh
Milioni 10 za shindano hilo nchini Tanzania. Anayeshuhudia kulia ni Meneja
Masoko wa Biko, Goodhope Heaven. Makabidhiano hayo ya fedha na kadi ya benki
kwa mshindi huyo yalifanyika Makao Makuu ya benki ya NMB kama sehemu ya
kumuandaa mshindi wa Biko kuzitumia fedha zake kwa uangalifu ili zimnufaishe
kiuchumi.
MSHINDI wa shindano la
bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Christopher Mgaya, jana
amepokea fedha zake sambamba na kupewa elimu ya kifedha kutoka Benki ya NMB
ambapo alifunguliwa akaunti ya kuhifadhia fedha hizo.
Mgaya alitangazwa
mwishoni mwa wiki katika droo ya kwanza ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10,
droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja akishirikiana na
mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Juhudi Ngolo, jijini Dar
es Salaam.
Nia ya kufunguliwa
akaunti katika tawi la NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam sambamba na
kupatiwa elimu ya kifedha kwa mshindi huyo limetokana na kiu ya kumuandaa kijana
huyo ili aweze kuzitumia ipasavyo fedha zake kwa ajili ya kumuinua kiuchumi
kutokana na uwapo wa mchezo wa bahati nasibu huo unaochezwa kwa kufanya miamala
ya kifedha kwenye Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money.
Akizungumza katika
ufunguzi wa akaunti ya mshindi wao huyo jana jijini Dar es Salaam, Meneja
Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwa mshindi wao wa Sh Milioni 10
wameona wasimuache hivi hivi badala yake wakaamua kumfungulia akaunti NMB
sanjari na kupatiwa elimu ya kifedha ili zimuendeleze kimaisha.
“Biko ushindi ni nje nje
kwa kuwa lengo letu ni kuwafanya Watanzania wafanikiwe kimaisha kwa kuutumia
vema mchezo wetu huu kwa kuingia kwenye kipengele cha lipa bili kwenye simu zao
za Mpesa, Tigo Pesa na Airtel Money kisha kuingiza namba ya kampuni 505050 na
kumalizia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456.
“Biko tunalipa kwa haraka
kwa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000,
500,000 na sh Milioni moja, huku zawadi ya ushindi wa Sh Milioni 10
inayopatikana kwa kuchezeshwa droo kila mwisho wa wiki italipwa kwa njia ya
hundi na kumuingizia fedha zake benki kama tulivyofanya kwa mshindi wetu Mgaya
aliyeibuka na ushindi kutokea Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam,” Alisema.
Naye Mgaya alisema kwamba
anawashukuru Biko kwa kumpatia zawadi yake kwa haraka sambamba na kumpeleka NMB
ili apatiwe elimu namna gani atazitumia fedha hizo ili zimuendeleze badala ya
kuzitumia kwa matumizi yasiyokuwa ya lazima.
“Wakati nashiriki kucheza
Biko sikutaraajia kama ningeshinda, lakini baada ya awali kushinda pia Sh 5000,
nilihamasika na kuendelea kucheza ambapo Jumapili sikuamini baada ya kupigiwa
simu na Kajala akinitaarifu kuwa nimeshinda Sh Milioni 10, ushindi ambao hakika
utanitoa sehemu moja kwenda nyingine hususan kwa kukamilisha ujenzi wa nyumba.
“Nawashukuru Biko huku
nikiwakumbusha Watanzania wenzangu kuchangamkia fursa ya bahati nasibu ya Biko
kwa sababu haiitaji kujua lolote zaidi ya kucheza kwa njia ya ujumbe wa simu na
kuingiza miamala kiasi cha Sh 1000 na kuendelea, huku kila Sh 1000 tunayolipa
ikitupatia nafasi mbili, zawadi za papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia
moja kwa moja kwenye droo ya kubwa ya wiki yakuwania Sh Milioni 10,” Alisema Mgaya.
Bahati nasibu ya Biko
imeanza kwa kasi kubwa nchini Tanzania, ambapo mbali na kumpatia zawadi yake ya
Sh Milioni 10 mshindi wao, pia inaendelea kulipa fedha mbalimbali walizoshinda
washiriki wao kwa haraka hali inayoongeza msisimko mkubwa kwa washiriki na
Watanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment