Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
amewataja watu 13 wenye mitambo ya kufyatua kazi za wasanii wa nje na ndani ya
nchi yetu wakutane kituo cha polisi cha
kati wakiwa na nyaraka halali za kufanyia kazi hiyo.
Akizungumza
na wasanii hao pamoja na wananchi leo katika mkutano wa kupambana na maharamia
wa kazi za wasanii,Makonda alisema kuna baadhi ya watu wanafanya kazi za bla
bla kwa kuwanyonya wasanii.
Amesema kuanzia leo ni mwisho kwa wale wanaouza
nyimbo za wasanii amesema wanaotakiwa kufanya hivyo niwale wenye mikataba
halali na wasanii wenye nyimbo husika.
Makonda amesema kuwa kazi zote za wasanii na
zinatakiwa ziwe na stika za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ilinchi iweze kupata
mapato na kukuza tasnia ya sanaa nchini.
Amesema kwa wale wanaouza kazi za wasanii mikononi
zinatakiwa kuwa na stika za TRA Pamoja na kuwa na kibali maalum kutoka bodi ya
filamu.
Hata hivyo amesema Makonda kunawatu wanafanya kazi
za kuwarubuni wasanii na na kufanya maisha yao yawe duni katika hiyo wakati
Nigeria inaongoza kwa kupata pesa nyingi kupitia filamu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia
Mjema akizungumza na Wasanii waliofika Kariakoo mara baada ya maandamano ya
kupinga Biashara ya uuzaji filamu za nje.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katikati akimsikiliza Katibu Mtendaji wa
Bodi ya Filamu Bi. Bi. Joyce Fissoo wakati akizungumza katika mkutano huo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda na baadhi ya
wasanii wa filamu, wasanii wa muziki pamoja na wasambazaji wa kazi za sanaa
wakiongoza maandamano ya kupinga uingizwaji wa filamu za kigeni nchini bila
kufuata taratibu
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda na baadhi ya
wasanii wa filamu, wasanii wa muziki pamoja na wasambazaji wa kazi za sanaa
wakiongoza maandamano ya kupinga uingizwaji wa filamu za kigeni nchini bila
kufuata taratibu
Baadhi ya wasanii waliohudhuria maandamano hayo
Kundi la Wasanii wakishangilia jambo
kutoka kwa mkuu wa Dar es Salaam Paul Makonda
Baadhi ya wasanii waliohudhuria kwenye maandamano hayo
wakishangilia jambo
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akisalimiana na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Kariakoo.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la
Filamu nchini, Jimy Mafufu akizungumza kwa niaba ya wasanii katika mkutano huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa
nchini (BASATA), Godfrey Mwingereza akizungumza na wasanii wa filamu waliofika
katika maandamano hayo yaliyoitimishwa katika mtaa wa Mafia Kariakoo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na Wasanii hao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda akizungumza na wasanii katika mtaa wa Mafya mara baada ya kumaliza
maandamano ya wasanii kupinga uuzwaji wa filamu za nje ambazo zinachangia
kushuka kwa thamani ya filamu za ndani kutokana na bidhaa hizo kutolipiwa kodi.
No comments:
Post a Comment