Dar Running Club ikishirikiana na Kampuni
ya maji ya kunywa Dasani, leo imeanza kufanya usajili kwa
washiriki wa mbio za km 10 na 21km zijulikanazo kama Dasani Marathoni
zitakazofanyika Jumapili ya Mei 14, 2017 jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya tatu sasa kwa Dar Running Club
kuendelea kuihamasisha jamii kufanya mazoezi kwa kuandaa mashindano haya,
ambayo yatafanyika tarehe Jumapili ya Aprili 2017.
Awali mashindano haya yalikuwa yakijulikana kama
May Day Marathon lakini kutokana na kushirikiana na kampuni ya maji ya Dasani
kuyaandaa mwaka huu yatajulikana kama Dasani Marathon 2017.
Akizungumzia mashindano haya, Mkurugenzi wa Mauzo
na Masoko wa Coca-Cola Kwanza LTD, kampuni ya inayotengeneza maji ya Dasani,
Nalaka Hettiarachchi amesema kuwa maji ya kunywa ya Dasani ni murua na yenye
kuondoa kiu, hususani wakati wa kufanya mazoezi au unapojisikia kuburudika na
ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki kwa wingi ili kujenga afya zao
kwa mazoezi.
Pia akiamini kuwa tunaweza kuleta uzoefu mkubwa kwa
washiriki na kulifanya kuwa tamasha la kukumbukwa. Pia tutalifanya tukio hili
kuwa maarufu zaidi na lakusisimua kwa miaka ijayo likiwa na vivutio vingi kwa
washiriki kutoka katika matembezi mbali mbali”. Lengo letu kubwa ni kusaidia
vijana na kuhamasisha Watanzania wenye vipaji kufikia viwango vya Kimataifa and
kuleta heshima kwa nchi yako… aliongeza Nalaka.
Kwa upande wake, rais wa Dar Running
Club, Goodluck Elvis, alisema kauli mbiu ya klabu yao ni "Active.
Wherever. Whenever" na imefarijika kuungana na Dasani katika
kuandaa mashindano haya Dasani Marathon 2017 ambayo umaarufu wake umekuwa
ukiongezeka kwa kasi mwaka hadi mwaka.
Kama ilivyokuwa kwenye mashindano ya miaka miwili
iliyopita, mbio hizo zitaanzia na kumalizikia Police Officers Mess
Oysterbay. Mbio za 21km zitaanza saa kumi na mbili kamili alfajiri, zikifuatiwa
na zile za 10km ambazo zitaanza saa kumi na mbili na nusu asubuhi. Washindi
watano wa mbio za 21km na washindi watatu wa mbio za 10km watazawadiwa zawadi
nono ikiwemo fedha taslimu.
Kiwango cha kusajili ni TZS 30,000/= kwa mbio zote
na mwisho wa usajili ni tarehe 13 Mei, 2017.
Vituo vya awali vya usajili vitakuwa
Colosseum Gym - Masaki, Shoppers plaza – Mikocheni, China Plaza: Ghorofa ya 11
mtaa wa Uhuru na Mheza Kariakoo na Mlimani City Mall. Washiriki wote
watafanikiwa kupata fulana zenye kiwango cha juu na vilevile watazawadiwa
medali pindi watakapokamilisha mbio hizo kwa wakimbiaji elfu moja wa kwanza.
Kwa
Taarifa Zaidi wasiliana na:
Goodluck Elvis, Dar
Running Club – President, 0715 302 336
Erick Kahwa, Dar
Running Club – Secretary, 0784024422
Dorothy Kipeja,
Dasani Marathon Marketing Manager – 0754 291 291
No comments:
Post a Comment