Tarehe 11 Aprili, 2017, Mhe. Balozi Wilson
Mutaganywa Kajumula Masilingi aliwasilisha hati za utambulisho kwa Mhe. Enrique
Peña Nieto, Rais wa Mexico, Ikulu Katika Jiji la Mexico.
Hafla hiyo ilishuhudiwa na Mhe. Luis
Videgaray Caso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Mexico na mke wa Mhe.
Balozi, Marystella Masilingi.
Wakati wa kuwasilisha hati hizo, Mhe. Balozi
alipata fursa ya kuongea na Mhe. Rais wa Mexico na kumpa salamu kutoka kwa Mhe.
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico akimpokea Mhe. Balozi Wilson M.
K. Masilingi, Balozi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mexico.
Katikati akitizama ni Mhe. Luis Videgaray Caso, Waziri wa Mambo ya Nje wa
Mexico.
Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico na Mhe. Balozi Wilson M.
Masilingi, Balozi mpya wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, nchini Mexico.
No comments:
Post a Comment