EXIM BANK YATOA MSAADA WA MADAWATI 50 MOROGORO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, April 6, 2017

EXIM BANK YATOA MSAADA WA MADAWATI 50 MOROGORO

Benki ya Exim Tanzania imetoa msaada wa madawati 50 yenye thamani ya milioni tano kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, madawati ambayo yatagawanywa kwa Shule ya Msingi Kisitwi na Chajware zilizopo wilayani humo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi madawati hayo, Meneja wa Exim Bank mkoani Morogoro, Patrick Njole alisema msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

“Exim Bank inapongeza jitihada ambazo zinafanywa na serikali za kuweka mazingira bora ya kujifunza na kwa kutoa msaada huu kwa shule za Morogoro, tunaamini itakuwa mwanzo wa kuelekea mbele zaidi kusaidia maeneo mengine nje ya miji mikubwa na kuyafikia maeneo ya vijijini,” alisema Njole.

Njole alisema wamekuwa wakiwekeza kwa muda mrefu katika sekta ya elimu na kuahidi kuwa benki ya Exim itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kusaidia kuboresha mazingira bora ya elimu ya Tanzania.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe aliishukuru benki ya Exim kwa msaada ambao wamewapatia kwa ajili ya kusaidia kupunguza changamoto ya uchache wa madawati unaowakabili katika mkoa wa Morogoro.


“Madawati ambayo mmetusaidia yatatusaidia kupunguza uhaba wa madawati ambao unatukabili katika shule zetu. Tunawaomba wadau wengine kufanya kama Exim Bank kusaidia mikoa ambayo bado ina tatizo hili,” alisema Mchembe.
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Bi Siriel Shaidi Mchembe akipokea madawati 50 yenye thamani ya shs milioni tano kutoka kwa Meneja Masoko wa Benki ya EXIM Tanzania Bw Abdulrahman Nkondo kama msaada kwenda kwa shule ya Kisitwi na Chakware za Mkoani Morogoro.
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Bi Siriel Shaidi Mchembe akiwa ameketi na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kisitwi wakati wa sherehe za makabidhiano ya madawati 50 kutoka kwa Benki ya EXIM Tanzania. Madawati yenye thamani ya shs milioni 5 yatagawanywa kati ya shule mbili; Kisitwi na Chakware za mkoani morogoro. Kulia ni Meneja Masoko wa Benki ya EXIM Tanzania Bw Abdulrahman Nkondo na kushoto ni Meneja wa Tawi la Benki hiyo Mkoani Morogoro Bw Patrick G Njole.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages