JE UNAUJUA MKATABA WA PANGO AMBAO NI LAZIMA KUSAJILIWA KISHERIA? - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, April 6, 2017

JE UNAUJUA MKATABA WA PANGO AMBAO NI LAZIMA KUSAJILIWA KISHERIA?


Kwa mujibu wa sheria ya usajili wa ardhi sura ya 334 ipo aina ya  mikataba ya pango ambayo baada ya kuwa imeingiwa kati ya mpangaji  na mwenye nyumba/eneo ni lazima  isajiliwe.  Mikataba  ya  aina  hiyo  isiposajiliwa  inakuwa   haijakidhi  vigezo  vya  kisheria  na  hivyo  kubatilika.

Aidha  pango  huhusisha  shughuli  mbalimbali.  Yapo  mapango  kwa  ajili  ya  biashara  maduka,  bar, mahoteli n.k.  na  pia  yapo  mapango  kwa  ajili  ya  makazi. Iwe  umepanga  kwa  ajili  ya  biashara  au  makazi  madhali  aina  yako  ya  upangaji  inahitaji  kusajiliwa  kisheria  basi  huna budi  kufanya  hivyo  ili  uhalali  wa  pango lako  upatikane.

Kabla ya kuona aina ya mikataba ya pango ambayo ni lazima kusajiliwa  ni vyema kujikumbusha kidogo kuhusu haki za mpangaji.

          1.   HAKI ZA MPANGAJI.

  (a) Haki ya kutoingiliwa na mwenye nyumba ili kumpa uhuru mpangaji  kufurahia pango lake.

    (b) Haki  ya kumpa  taarifa(notice)  mapema  mpangaji  ikiwa mwenye nyumba  anataka  kukagua  nyumba/eneo  lake.

   (c)  Haki  ya  kutoondolewa  au  kusitishiwa  mkataba  mpaka  baada ya  kupewa  taarifa  maalum( notice) .

    (d) Haki  ya  kuambiwa  ukweli  kuhusu  hali  ya  nyumba kabla  ya  kusaini  mkataba  wa  pango. Mfano  kuambiwa  ikiwa  eneo  linajaa  maji  kipindi  cha  mvua, kuambiwa  ikiwa  nyumba  inavuja n.k.

     (e)  Haki ya kukataa sharti lolote ambalo linalenga kuminya uhuru wa mpangaji au linalovunja sheria yoyote ya Tanzania.

    (f)  Haki ya kupewa taarifa mapema (notice) kabla ya kupandisha  kodi ya pango.

      (g) Haki ya kupewa taarifa mapema (notice) kabla ya kubadilisha sharti lolote katika mkataba wa pango.

Haki  ni  nyingi  hizi  ni  baadhi  tu.

       2.   MKATABA WA PANGO AMBAO NI LAZIMA KUSAJILIWA

Kifungu cha 54 (1) cha Sheria ya Usajili wa Ardhi, Sura ya 334 kinasema kuwa pango ambalo mkataba wake unazidi miaka mitano linatakiwa kusajiliwa.

Wapo watu wanapanga mahoteli, bar, maduka nk. ambao miaka ya  pango katika makubaliano yao ni zaidi ya mitano. Hawa mikataba  yao  ni lazima isajiliwe.  

Mara nyingi mkataba  wa  pango  huweza  kuwa   wa  miaka  mingi  kutokana  na aina ya biashara anayotaka kufanya mpangaji halikadhalika uwekezaji  anaotarajia kufanya eneo analotegemea kupanga. Wakati mwingine  mpangaji hukubaliana na mwenye eneo kufanya marekebisho  makubwa (renovation) ili  eneo lifanane na aina ya biashara anayotaka kufanya. 

Mbali na hayo ni vema kufahamu pia kuwa mkataba ambao ni chini  ya  miaka mitano lakini mkataba huo una sharti la kuhuisha (renew) kwa  miaka  mingine, ambapo ukijumlisha miaka ya awali na hiyo ya  kurenew jumla inazidi mitano basi nayo ni lazima kusajiliwa.

Tumeongelea  mikataba  inayozidi  mikaka  mitano  lakini  hatupaswi  kusahau kuwa hata mikataba ya pango iliyo chini ya miaka mitano inaweza kusajiliwa japo sio lazima.  Mikataba hii una chaguo kusajili au  kutosajili. Kisheria kutosajiliwa kwake kwa namna yoyote hakuathiri  uhalali wake.

3.  WAPI  UKASAJILI.

Msajili  wa  nyaraka  anayepatikana  ofisi  za  ardhi  ndiye  anayehusika  na usajili wa  mikataba  hii. Unapofika  ofisi  yoyote ya ardhi  utapewa  maelekezo lipi la kufanya ili mkataba wako uweze kusajiliwa.


Aidha ipo ada ya kulipa kabla ya usajili ikiwemo kodi ya faida.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages