Filamu hiyo, ambayo ni
ya nane katika mwendelezo wa filamu za Fast & Furious, ilipata mauzo ya
jumla ya $532.5m (£424.7m) duniani wikendi
ya Pasaka.
Hayo ndiyo mauzo ya juu
zaidi duniani kwa filamu yoyote siku zake za kwanza baada ya kuzinduliwa rasmi.
Filamu hiyo imepita
mauzo ya $529m (£421.8m) rekodi ya awali
iliyowekwa na Star Wars: The Force Awakens.
Mauzo hayo ya filamu
hiyo nchini Marekani hata hivyo yalikuwa chini ukilinganisha na mauzo ya filamu
iliyotangulia.
Furious 7 ilipata mauzo
ya $147.2m (£117.3m) nchini Marekani
ilipozinduliwa 2015.
Lakini filamu ya sasa
imezoa $100.2m (£80m) pekee.
Licha ya kushuka kwa
mauzo yake Marekani, filamu hiyo bado ilichangia sehemu kubwa ya mauzo ya
filamu Marekani, ambapo ilichangia karibu theluthi mbili.
Mshindani wake wa karibu
alikuwa The Boss Baby, ambayo iliuza $15.5m na kuwa ya pili.
Filamu za Fast &
Furious zilianza kuuzwa 200.
Ufanisi wa filamu hii ya
sasa ulichangiwa sana na China ambapo mauzo yake yalikuwa $190m (£151m) kwa siku hizo
tatu.
Vin Diesel, ambaye
ameigiza katika kila filamu ya Fast & Furious amesema anashukuru sana na
amefurahishwa sana na ufanisi wa filamu hiyo.
Wengine walioigiza
katika Fate of the Furious ni Charlize Theron, Tyrese Gibson na Ludacris.
Filamu nyingine za
Furious zitatolewa mwaka 2019 na 2021.
No comments:
Post a Comment