Sarah Ikumu, 16,
aliyezaliwa Uingereza, aliwashangaza wengi katika kipindi cha vipaji cha
Britain's Got Talent, alipoimba wimbo wa And I'm Telling You ambao
unadaiwa kuwa mgumu sana kuuimbwa ipasavyo.
Wimbo huo wake Jennifer
Holliday ulitumiwa kwenye filamu ya Dreamgirls iliyotolewa mwaka 2006.
Uimbaji wa Sarah
uliwaacha waliohudhuria mashindano hayo wakiwa wameduwaa huku wote wakisimama
na kumshangilia.
Kilele cha uimbaji wake
kikifika pale mmoja wa majaji ambaye anajulikana kuwa mgumu kufurahisha, Simon
Cowell, alipobonyeza kengele ya dhahabu ambayo humpeleka mshiriki moja kwa moja
hadi nusu fainali ya mashindano hayo.
Sarah ambaye anasomea
Milton Keynes alianza kuimba akiwa na miaka mitano huku akishiriki kwa
mashindano kadha ya nyimbo.
Lakini hili ndilo
shindano la kwanza ambalo anasema kuwa ni ndoto ambayo imetimia, mwanzo pale
Jaji Simon alipompongeza kwa talanta yake akimuambia "lilikuwa jambo la
kushangaza kwa mtu rika lake kusimama mbele ya watu akiwa na hofu na kuelekea
kuimba wimbo ni kama ameutunga mwenyewe".
Mwimbaji mashuhuri
ambaye pia ni jaji Alesha Dixon alimwambia Sara kuwa "'hakubaliwi' kuwa na
talanta kama hii katika umri wake"
Majaji wengine wawili
wakiwemo David Williams, Amanda Holden pia walimmiminia pongezi.
Mitandao ya kijamii
ilifurika watu wakimsifu.
No comments:
Post a Comment