Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
limeandaa hafla maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya timu ya
Serengeti Boys inayojiandaa kucheza fainali za kuwania Kombe la Afrika kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini Gabon. Fainali hizi zitafanyika
kufanyika kuanzia Mei 14 hadi 28, 2017.
TFF inatambua kuwa wadau mbalimbali wamekuwa
wakichangia timu hiyo kupitia mitandao ya simu kama vile namba 0687 333 222
kadhalika Selcom kwa namba 22 33 44 pia kuweka fedha kwenye akaunti Na. 00 866
280 03 katika Benki ya Diamond Trust (DTB).
Sasa siku ya Ijumaa Aprili 28, 2017 TFF imeandaa
hafla maalumu ya kupokea michango hiyo, lakini pia kuchangisha fedha zaidi
maana lengo ni kukusanya shilingi bilioni moja (Sh. 1 Bil.) Hafla hiyo
itafanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.
TFF imeamua kutumia fursa kuwakaribisha wawakilishi
wa makundi mbalimbali ili wawasilishe michango yao na kumkabidhi mgeni rasmi.
Kwa kutambua michango mbalimbali ambayo imekusanywa
kupitia makundi ya mitandao ya jamii kama WhattsApp, facebook hivyo TFF inaomba
wawakilishi wa makundi yote ya mitandao ya jamii (admins) ambao wamekusanya
michango hii wajiorodheshe ili wapate fursa ya kukabidhi michango ya makundi
yao kwa mgeni rasmi katika hafla hii.
Admins hawa wanaombwa wajiorodheshe kwa kutuma
email kwenda fdf@tff.or.tz, kwa kupiga simu
0787 176767 au kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda 0787 176767 ambayo pia
inapatikana kwenye mawasiliano ya WhattsApp.
Aidha wawakilishi wa makundi mengine kama idara za
Serikali, mashirika ya umma na binafsi kadhalika watu binafsi ambao nao
wamechangia nao pia tunaomba wajioredheshe ili wapewe fursa pia ya kukabidhi
michango yao siku hiyo ya Ijumaa.
TFF inashukuru sana kwa ushirikiano.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu ibariki Serengeti Boys
No comments:
Post a Comment