HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYONOGA KATIKA UZINDUZI WA WASATU NORTHAMPTON-UINGEREZA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, April 8, 2017

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYONOGA KATIKA UZINDUZI WA WASATU NORTHAMPTON-UINGEREZA

Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilizunduliwa kwa vigelegele na muziki mjini Northampton, katikati ya Uingereza jumamosi ya tarehe 1 April 2017.

Tafrija hiyo ndogo lakini iliyowakutanisha zaidi ya Watanzania mia moja na marafiki zao wa Kenya, Uganda, Kongo, Nigeria, Uingereza nk, ilihudhuriwa na Mheshimiwa Balozi Dk Asha Rose Migiro.

WASATU ilibuniwa mwaka jana kati ya wasanii wakiongozwa na mwanamuziki na mcheza sarakasi Fab Moses na promota wa vyakula vya Kitanzania, Bi Neema Kitilya. Asilimia 20 ya kipato cha onesho zilitolewa na WASATU kwa waliofikwa maafa ya mafuriko ya maji karibuni Tanzania.
 Watanzania na marafiki zao wakijimwaga ukumbi wa The Eastern District Social Club, Northampton.
 Furaha na shangwe ya WASATU
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dk Asha Rose Migiro (katikati) na mwana WASATU - Mcheza ngoma asilia, Khadija Ismail. Wa kwanza ni Mtanzania, Salma Kashinde
 Muziki motomoto, Northampton
 Bango la shughuli hiyo lilikuwa hivi
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dk Asha Rose Migiro akihutubia tafrija hiyo
 Mpiga saksafoni mkongwe na mwanaWASATU- RamaSax- mzawa wa Tanga akipuliza vituz
WASATU: Toka kushoto nyuma, Rama Sax, Saidi Kanda, John Londo, Fab Moses , Freddy Macha Mbele : Khadija Ismail na Neema Kitilya.
 Vitumbua vya Neema Kitilya
 Nyama Choma
 Mwana WASATU Fab Moses akionesha vituko vyake vya Sarakasi
Mwanamuziki wa Kikongo aliyehamia Tanzania miaka mingi, Kawele Mutimanwa na bendi ya “Afrika Jambo” jukwaani Northampton
Mwanamuziki mlemavu na msanifu picha, Kea , toka Kenya aliyetengeneza tangazo la WASATU 
Mwanamuziki wa Kikongo Mboka Lia (anayejulikana kwa jina “Burkina Faso”) ndani ya nyuzi na sakata sakata la WASATU
Mwanamuziki mlemavu aliyekomaa - mtunzi, mwimbaji na mpiga gitaa hatari, John Londo – mwana WASATU aliyebobea. Kileleni Northampton bila kukosa.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages