KIWANDA CHA SARUJI CHA SIMBA CEMENT YAIPIGA TAFU JUKWAA LA WAHARIRI MILIONI 14 - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, April 8, 2017

KIWANDA CHA SARUJI CHA SIMBA CEMENT YAIPIGA TAFU JUKWAA LA WAHARIRI MILIONI 14


Tanga, KIWANDA Cha Saruji cha Simba Cement Tanga, kimesema moja ya faida yake imekuwa ikiipeleka katika masuala ya kijamii yakiwemo, Afya, Mazingira na Elimu.

Akizungumza mara baada ya Wahariri (Jukwaa la Wahariri TEF) kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda cha Saruji kujionea shughuli ambazo zinafanywa, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Renhardt Swart, alisema moja ya faida huipeleka kwa wananchi.

Alisema wamekuwa wakisaidia madawati, mifuko ya saruji na majengo pamoja na vyoo kwa shule ambazo zimekuwa zikihitaji msaada. Akikabidhi shilingi milioni 14 kwa Jukwaa hilo, Swart alisema pesa hizo zinaweza kuwasaidia katika majukumu yao mbalimbali ukiwemo mkutano mkuu ambao unaendelea Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Makamo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deudas Balile, alisema amefurahishwa na uzalishaji wa Saruji pamoja na mipango kabambe kiwandani hapo.

Akizungumzia msaada huo, Balile alisema utasaidia katika masuala mbalimbali ya Jukwaa hilo ikiwa na pamoja na mkutano mkuu na kutoa shukurani na kuwataka wawekezaji wengine kuiga mfano kama huo.



Afisa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Beni Lema na Meneja Mawasiliano na Uhusiano Bi Mtanga Noor wakiwakaribisha Wahariri wa Vyombo vya habari waliokitembelea kiwanda hicho.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Bi Mtanga Noor akiwakaribisha Wahariri wa Vyombo vya habari waliokitembelea kiwanda hicho.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Bi Mtanga Noor wakiteta jambo na mmoja wa wahariri wa habari waliokitembelea kiwanda hicho.

Afisa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Beni Lema akiwakaribisha na kuwaongoza wahariri wa vyombo vya habari waliokitembelea kiwanda hicho.
Afisa mmojawapo wa kiwanda hicho akimkaribisha mhariri wa vyombo vya habari waliokitembelea kiwanda hicho.

Wahariri wa vyombo vya habari waliokitembelea kiwanda hicho wakiwa katika kusubiri maelekezo kutoka kwa wenyeji wao.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Bi Mtanga Noor akiwakaribisha na kutoa utambulisho kwa wahariri wa Vyombo vya habari waliokitembelea kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Renhardt Swart, akielezea jambo kuhusiana na Kiwanda hicho kwa wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kiwanda hicho.
Mmoja wa Maafisa wa kiwanda hicho akifurahi jambo lililozungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Renhardt Swart.

 Wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kiwanda hicho wakifuatilia taarifa inayotolewa na Mkurugenzi wa Kiwanda hicho.

Wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kiwanda hicho walipata nafasi kuhoji na kuuliza maswali mbalimbali kuhusu kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Renhardt Swart. akiwa anatoa maelezo ya majibu ya maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kiwanda hicho.

Afisa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Beni Lema akifuatilia kwa makini taarifa inayotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Renhardt Swart kwa wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea kiwanda hicho.
Makamo Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri wa Habari (TEF), Deudatus Balile (kulia), akipokea mfano wa hundi wa shilingi milioni 14 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji kiwanda cha Saruji cha Tanga Simba Cement, Renhardt Swart, kusaidia jukwaa hilo katika majukumu yake ya kila siku ikiwemo mkutano wao mkuu unaoendelea Mkoani Kilimanjaro.


Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Renhardt Swart, Afisa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Beni Lema na mmoja wa maofisa wa kiwanda hicho wakiteta jambo.
Mmoja ya wahariri akipokea mfano wa hundi wa shilingi milioni 14 kutoka kwa Afisa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Beni Lema kusaidia jukwaa hilo katika majukumu yake ya kila siku ikiwemo mkutano wao mkuu unaoendelea Mkoani Kilimanjaro.


Afisa Mawasiliano na Masoko kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Tanga, Hellen Maleko, (kulia) akiwakabidhi hundi yenye mfano wa shilingi milioni 14 Wahariri wa Jukwaa la vyombo vya habari mara baada ya kutembelea kiwanda hicho ikiwa ni msaada katika mambo yao mbalimbali ukiwemo mkutano wao mkuu unaoendelea Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Wahariri kutoka vyombo mbalimbali wakiangalia eneo la uchimbaji wa Material Kware kilometa 2 kutoka ndani ya eneo la kiwanda.
 Eneo la Kware ambalo kiwanda hicho toka kianze uzalishaji wamekuwa wakichimba Matirial hadi hii leo ambapo Afisa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Beni Lema amewaambia Wahariri hao kuwa kuna kiwango kikifika watasimamisha uchimbaji na kuanzisha mradi wa Ufugaji Mamba.
Afisa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Beni Lema akielezea jambo kwa Wahariri waliotembelea machimbo hayo

Wahariri kutoka vyombo mbalimbali wakiangalia eneo la uchimbaji wa Material Kware kilometa 2 kutoka ndani ya eneo la kiwanda.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages