
MUONEKANO wa Majengo ya Hotel ya Sandies Nungwi Beach Resort iliyowekwa jiwe la msingi la mradi wa ujenzi huo wa hoteli, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, leo 26-2-2025 Mkoa wa Kaskazini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Wawekezaji wa Mradi wa Hoteli ya Sandies Nungwi Beach Resort, alipowasili katika viwanja vya hoteli hiyo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa hoteli hiyo leo 26-2-2025, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe.Shariff Ali Shariff.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya kitaalamu ya ujenzi wa Hoteli ya Sandies Nungwi Beach Resort kutoka kwa muwekezaji Paolo Rosso, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa hoteli hiyo, uliyofanyika leo 26-2-2025, Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia la uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Hoteli ya Sandies Nungwi Beach Resort Zanzibar na Muwekezaji wa Mradi huo, Mr.Burgio, (kushoto) hafla hiyo iliyofanyika leo 26-2-2025 Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe. Shariff Ali Shariff.









No comments:
Post a Comment