MWANAFUNZI ESTHER BARUA AMFURAHISHA Dkt. SAMIA, ARUHUSIWA KUKALIA KITI CHA RAIS - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, February 27, 2025

MWANAFUNZI ESTHER BARUA AMFURAHISHA Dkt. SAMIA, ARUHUSIWA KUKALIA KITI CHA RAIS

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Magila ya Muheza Ester George Barua ambaye alimruhusu akalie kiti chake cha Rais kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa CCM Jitegemee Wilayani Muheza Mkoani Tanga tarehe 27 Februari, 2025. Rais Dkt. Samia alifurahishwa na Mwanafunzi huyo wa Shule ya Sekondari ya Serikali ya Kata (Magila Sekondari) wakati akielezea mafaniko ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa Lugha ya Kingereza.
Ester ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Magila, Wilaya ya Muheza, Mkoa wa Tanga; mmoja kati ya wanafunzi waliofika kumsalimia Rais na kumueleza namna uwekezaji uliofanywa na Serikali katika elimu kwa majengo mapya, walimu na vifaa vya kufundishia unavyoboresha maisha yao shuleni, na kuwapa matumaini ya kufikia ndoto zao. 

Katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024, serikali imeweza kujenga shule mpya za msingi 1,649 na shule mpya za sekondari 1,042 nchi nzima. Kazi hii imekwenda sambamba na kuboresha mtaala na Sera ya Elimu ambayo ilizinduliwa rasmi Februari 1 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages