Maafisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Watembelea Vituo vya Uandikishaji Wapiga Kura Wapya Kaskazini B Unguja - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, February 27, 2025

Maafisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Watembelea Vituo vya Uandikishaji Wapiga Kura Wapya Kaskazini B Unguja

Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Idirisa Haji Jecha (kushoto) akitoa Ufafanuzi kwa Mawakala wa Vyama kuhusiana na Baadhi ya Changamoto zilizojitokeza katika Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura wapya wakati walipofanya ziara kutembelea Kituo Cha Uandikishaji Shehia ya Kisongoni Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Idirisa Haji Jecha (kushoto katikati) akimsikiliza Mmoja kati ya Mawakala wa Vyama akizungumzia Changamoto zilizojitokeza katika Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura wapya wakati Makamishna walipofanya ziara kutembelea Kituo Cha Uandikishaji Shehia ya Kisongoni Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Makamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar wakiwa katika Kituo cha Uandikishaji wapiga Kura wapya Shehia ya Kiwengwa wakati walipofanya ziara kutembelea Vituo mbalimbali vya Uandikishaji Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Idirisa Haji Jecha akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Ziara Maalum ya Kutembelea Vituo mbalimbali vya Uandikishaji Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Na Rahma Khamis, Zanzibar

Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Idrisa Haji Jecha ameushukuru Uongozi wa Wilaya Kaskazini B, na wananchi wake kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura.

Shukurani hizo amezitoa huko Skuli ya Kiwengwa Wilaya ya Kaskazini B, ikiwa ni muendelezo mwa ziara ya kutembelea vituo vya uandikishaji wapiga kura awamu ya pili.

Amesema zoezi hilo limefaniikiwa kwa kiasi kikubwa kwani walikadiria kuandikisha wananchi 3713 lakini wamefikia kuandikisha wananchi 5815 hadi kufikia majira ya mchana.

"Hali hii inaonyesha wananchi wanaopiga kura wamehamasika sana hata ikifika muda wa kufunga vituo naamini idadi itaongegeka zaidi" alisema Kamishna.

Nao Wakuu wa vituo vya uandikishaji akiwemo Nihifadhi Faki Ali kutoka Pangeni wilayani humo wamesema kuwa hadi kufikia leo zoezi linakwenda vizuri na hakuna tatizo lolote wanafanya kazi kwa mashirikiano ili kufikia lengo lililolotarajiwa.

Akizungumzia kuhusu changamoto zilizojitokea katika vituo hivyo wameeleza kuwa ni baadhi ya watu vidole vyao kutosoma katika mashine lakini tatizo hilo limefanyiwa marekebisho na wananchi wanaendelea kupatiwa huduma kama bila ya usumbufu wowote.

Jumla ya Vituo 32 vimetembelewa Wilayani humo ikiwemo Kinyasini, Mgambo Kisongeni, Pangeni, Kilombero na Upenja ambapo zoezi hilo limekwenda vizuri na linatarajiwa kumalizika leo Febuary 27 katikaWilaya hiyo ya Kaskazini ‘B’.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages