Idadi ya wabunge
waliopewa vitisho na watu wasiojulikana imezidi kuwa hadharani baada ya majina
ya wabunge wengine wanne wapya kutajwa bungeni kuwa ni miongoni mwa wabunge
ambao maisha yao yapo hatarini na hivyo wanaliomba bunge kushughulikia usalama
wao kwani hawajui kwa sasa watafanyaje ili kujinusuru kutoka katika hatari
hiyo.
Wakiomba miongozo ya kiti
Mhe. Mwita Waitara mbunge wa Ukonga alitaja majina ya wabunge wanne ambao
alitumiwa majina kupitia ujumbe wa mfupi wa simu kuwa wanasakwa huku Mhe. Dkt.
Godwin Molley mbunge wa Siha naye aliomba muongozo wa kiti kutaka bunge
liahirishwe ili wajadili hali hiyo hata hivyo kiti kilikataa miongozo hiyo.
Mhe. Said Kubebea ni
mbunge kutoka Ubungo ambaye anasema kilio cha wabunge kuhusu kuhakishiwa
usalama wao ni jambo ambalo mtu yoyote hapaswi kukipuuza kauli ambayo
inaongezewa nguvu na Mhe. Mwigulu Nchemba waziri wa mambo ya ndani ya nchi
anasisitiza usalama upo huku waziri wa habari utamaduni sana na michezo Mhe.
Dkt. Harrison Mwakyembe akimjibu Mhe. Juma Mkamia kuhusu yeye kushiriki mkutano
wa mwanamuziki Roma Mkatoliki.
Katika hatua nyingine
wabunge wamepata nafasi ya kuchangia hotuba ya waziri mkuu ikiwa ni katika
hatua za kuhitimisha ambapo wabunge wengi wamesema kama bajeti itatekelezwa
kama ilivyopangwa itakuwa msaada mkubwa.
No comments:
Post a Comment