Mbunge wa jimbo la
Chalinze, Ridhiwani Kikwete anamshangaa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu
Nchemba kuendelea kukaa kimya juu ya matatizo ya kiusalama kwa wananchi
yanayoendelea nchini wakati yeye ndio kiongozi mwenye dhamana ya kulitatua
hilo.
Akiongea bungeni Jumanne
hii, mbunge huyo amesema, “Kumekuwa na malalamiko mengi sana, tumeshuhudia
malalamiko mengine yanahitaji majawabu kama siyo majibu ya haraka ili kuondoa
hizi sintofahamu walizonazo wananchi.”
“Niwaombe sana hakuna
sababu ya mtu kama Mhe. Waziri Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati wananchi
wanalalamika juu ya hali yakiusalama katika maisha yao,” ameongeza.
“Mimi binafsi niishauri
serikali yangu kwamba unapojibu jambo lolote lile unatoa hali ya wasiwasi,”
amesisitiza.
No comments:
Post a Comment