Zaidi ya heka mbili za mashamba ya mahindi ya watawa wa Lighano Jimbo kuu katoliki la Songea yamefyekwa na kundi la vijana wanaodaiwa kukodiwa na bwana David Milinga waliovamia mashamba na kufanya uharibifu huo.
Zaidi ya heka mbili za mashamba ya mahindi ya wataa a Lighambo
Jimbo Kuu Katoliki la songea, yamefyekwa na kundi la vijana wanaodaiwa kukodiwa
na Bwana david Milinga waliovamia mashamba na kufanya uharibifu huo.
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Namtumbo ilitembelea
mashamba yaliyoharibiwa na kuona mahindi yalivyofyekwa mlezi wa nyumba ya
watawa padre Michael Milinga amesema mara kadhaa walikuwa wanapokea simu na
ujumbe wa vitisho kutoka kwa bwana mmoja aliyetajwa kwa jina la David Milinga
ya kuwa wakilima yeye atakwenda kuvuna juzi walipokea taarifa kutoka kwa
mwananchi mmoja kuwa kundi la vijana kutoka kijiji cha mkongo wakiwa na mapanga
wanafyeka mahindi.
Aidha mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Luckness Amlima amelishangaa
jeshi la polisi wilayani humo kutochukua hatua kwa Zaidi ya siku tatu toka uharibifu
huo ufanyike.
Baada ya kamati ya ulinzi kuondoka eneo la tukio mtuhumiwa David
Milinga na kundi la vijana ambao idadi yake haikufahamika walikamatwa na
kufikishwa kituo cha polisi wilaya ya Namtumbo.
No comments:
Post a Comment