Mradi wa Ujenzi wa Mabweni unaosimamiwa na Wakala wa Ujenzi
Tanzania (TBA), uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam unatarajiwa kukamilka hivi
karibuni.
Hayo
yamesemwa mapema hii leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda mara
baada ya kufanya ziara ya ukaguzi katika mradi huo.
Amesema
kuwa kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa mabweni hayo kutapunguza gharama kubwa
ambayo wamekuwa wakiipata wanafunzi wa chuo hicho kupanga vyumba mitaani.
Aidha,
Makonda ameongeza kuwa anajisikia fahari kubwa kufanya kazi chini ya Rais Dkt.
John Magufuli kwa kuwa anatimiza ahadi zake za kukamilisha Miradi mbalimbali
katika Jiji la Dar es salaam ukiwemo mradi wa ujenzi wa mabweni hayo ya
wanafunzi katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.
Mabweni 20 ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye
uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,840 yaliyounganishwa kimuundo wa ghorofa nne,
yanatarajiwa kusaidia kupunguza gharama za malazi kwa wanafunzi wengi wa chuoni
hapo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akisalimiana na Afisa Mahusiano wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jackson Isdory alipotembelea na kukagua majengo
ya hostel za wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), yanayojengwa na Wakala
wa Majengo Tanzania (TBA) mapema leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akipatiwa maelezo na mmoja wa wakandarasi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akitaka kujua jambo kutoka kwa Afisa
Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jackson Isdory kuhusu maendeleo ya
ujenzi wa majengo hayo alipotembelea na kukagua majengo ya hostel za wanafunzi
wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), yanayojengwa na Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) mapema leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akikagua baadhi ya Vitanda vilivyopo katika Hosteli hizo, mapema leo.
Afisa
Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jackson Isdory akifafanua jambo
kuhusu maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh
Paul Makonda alipokwenda kutembela na kukagua majengo hayo.
Baadhi ya majengo ya hosteli za wanafunzi wa UDSM zinazojengwa.
Meya
wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta akijadili jambo na baadhi
ya wawakilishi na viongozi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akiongea na waandishi wa habari alipotembelea na kukagua majengo
ya hostel za wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), yanayojengwa na Wakala
wa Majengo Tanzania (TBA) mapema leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akikagua baadhi ya Bafu na Vyoo vilivyopo katika Hosteli hizo, mapema leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akitoa maelekezo kwa afisa
Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jackson Isdory.
No comments:
Post a Comment