Tamasha
kubwa la muziki la MTN Bushfire, kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika nchini Swaziland
kuanzia Mwezi Mei 26 – 28. 2017, ambapo likitarajia kukusanya watu mbalimbali kutoka
Duniani kote ambao watajumuika pamoka kufurahia na kucheza muziki mzuri kutoka
kwa wasanii na bendi za pande zote za dunia.
MTN
Bushfire ni miogoni mwa tamasha kubwa la muziki na lenye mvuto zaidi
linalifanyika Afrika.
Aidha
miongoni mwa listi ya wasanii watakaotumbuza jukwaani kwa mwaka huu ni pamoja
na 80 Script (Swaziland), Baloji (congo), Ben day & the concrete lions
(Afrika Kusini), Bombino, Chico Antonio (Msumbiji), Dj Bob (Afrika Kusini),
Faada Freddy (Senegali/Ufaransa), Femi Koya, Flame Boy universe (Swaziland),
Goodluck (Afrika Kusini), Gren Seme.
Wengine ni
Kwesta, Matthew Mole, Michael Canfield,Msaki, Petite Noir ,The
Jaigermeister brass Cartel ft. Reason, Rootsword, Sands, Seba Kaapstad,
Siyinqaba, The Kiffness, Hugh Masekela, Jah Prayzah, Jeremy Loops, Jojo Abot,
Kids n Cats na Mkongwe wa Kwaito kutoka Afrika Kusini Tkzee.
Tamasha la
MTN Bushfire ni linadhaminiwa na MTN huku likiwa ni miongoni mwa matamasha 7
makubwa Barani Afrika ambayo umvutia mtu kiuhalisia kwa mujibu wa CNN huku pia likitajw
akuwa ni miongoni mwa matamasha 10 bora ya Kimataifa kipindi cha Summer.
Moja ya maonyesho ya
tamasha hilo yaliyopita
No comments:
Post a Comment