Benki ya NMB kwa
kupitia tawi lake la NMB Zanzibar imeandaa hafla na kuwakusanya wateja wake
wadogo na wakati ambao ni wanachama wa klabu ya biashara ijulikanayo kama “NMB Business Club”
ili waweze kuzungumza nao katika ufanikishaji wa biashara zao lakini pia kutoa
mafunzo ya kibishara. Hafla hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi na Meya wa Manispaa
ya Mjini Zanzibar, Khatibu Abdulrahman Khatibu ilifanyika mwishoni mwa
wiki na kuhudhuriwa na wafanyibiashara zaidi ya 200 wa mjini Unguja.
Kusudi kubwa la
hafla hii ni kutaka kusikia kutoka kwa wafanyabiashara wa mjini Zanzibar
mahitaji waliyokuwa nayo lakini pia kuwapa semina elekezi ili kufikia malengo
ya bishara zao.Ingawa Benki ya NMB imekua na utamaduni wa kukutatana na wateja
wake wa Nyanja tofauti tofauti katika nyakati tofauti ili kuwaelezea maendeleo
na huduma mbali mbali ambazo NMB inakua imezifikia kwa kusudi la kurahisisha
huduma za kibenki kwa wateja wake.
“Sisi kama NMB tunayofuraha kubwa sana na tunajivunia
kuwa na wateja wetu leo na tunaamini kwa kupitia mkutano huu na mafunzo ambayo
leo mmeyapata yatakuwa mwongozo kila mnapofikiria kukua kibishara zaidi sana
nawasihii mzingatie yale yote yaliyotolewa na watoa maada lakini zaidi
mzingatie wosia wa mgeni rasmi Mheshimiwa Khatibu. Naamini mkiwa na
nidhamu katika matumizi ya fedha hasa mikopo ambayo mnayohukua mtafika mbali
kibiashara,” alisema Vicky
Bishubo, Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam.
Nae mgeni rasmi
katika hafla hii Mhe. Khatibu Abdulrahman Khatibu aliwasihi sana
wafanya biashara hao kua na nidhamu ya Mikopo inayochukuliwa .Alisema
wengi wa wafanya biashara hupotoka mara wanapopata mitaji ya bishara zao
hudhani kua pesa itabakia katika mikono yao siku zote.Aidha aliupongeza uongozi
wa benki ya NMB kwa kuona haja ya kuwa na klabu ya biashara ambayo kusudi lake
ni kuwa karibu na wateja wao ili kuhakikisha wanafikia malengo ya biashara zao.
“Kwanza kabisa ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa
uongozi mzima wa benki ya NMB nkwa kuona umuhimu wa kuwa na klabu ya biashara
hapa Mjini Unguja . Klabu hiii iwe chachu ya maendeleo kwenu wafanyabishara wa
Zanzibar ili kusudi hata wale ambao wamekua waoga wa mikopo na waoga wa
kufanya biashara wapate ujasiri kutoka kwenu.Lakini pia nitoe angalizo kwenu
wafanya biashara , Msibweteke na pesa mnazozipata msidhani pesa hizo zitakaa
mikononi mwenu siku zote. Mnatakiwa kuwa na nidham katika matumizi yenu ya Pesa
Mafunzo mnayopewa yakawafae ili muweze kufikia malengo ya Biashara zenu,” alisema Khatibu Abdulrahman Khatibu.
Benki ya NMB
imfanikiwa kuzindua klabu za bishara (Business Clubs) katika mikoa yote
nchini. Ili kuhakikisha kuwa wanakua karibu na wateja wake NMB imekua ikifanya
mikutano na wanachama wa klabu hizi kila mwaka ili kusikia changamoto amabazo
wanakutana nazo.Lakini pia kuwaelezea wateja wao uboreshwaji wa huduma mbali
mbali za kibenki ambao NMB umefanya.NMB wanatoa wito kwa wateja wao
kutokua waoga wa kufanya biashara na kuchukua mikopo Benki.
No comments:
Post a Comment