Mama mzazi wa
aliyekuwa nyota wa filamu bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa
siku ya kumbukumbu ya mwanaye makaburini Kinondoni, alimfyatukia msanii wa
filamu nchini, Vincent Kigosi ‘ray’ aliyekuwa swahiba wa mwanaye kuwa,
hajawahi kumuona hata siku moja makaburini hapo kuomboleza kifo cha mwanaye miaka
yote ambayo hufanya kumbukumbu hiyo.
Akizungumza na Wor’Out
Media makaburini hapo, Aprili 7, mwaka huu, mama Kanumba alisema kuwa,
tangu aanze kuazimisha kumbukumbu za mwanaye hajawahi kumuona Ray
akiomboleza wala hata kuungana naye makaburini kama mastaa wengine wanavyofanya.
“Yaani sijawahi kumuona huyo Ray akijumuika na sisi makaburini, utadhani yeye
ataishi milele duniani.
Kumbuka somo la leo
kutoka kwenye Biblia linatufundisha kuwa, kila binadamu atakufa,” alisema mama
Kanumba. Aidha, mama huyo alisema kuwa kama Ray na mwanaye waliwahi kuwa na
ugomvi basi amsamehe kwani binadamu tumefunzwa kusamehe na sasa hayupo tena
duniani.
“Unajua huenda
walikoseana marehemu akiwa hai lakini mpaka leo naona kama ana kinyongo,
asamehe tu. Naongea hayo kwa sababu sijawahi kuona akimuenzi hata kwa kufika
makaburini kuungana na sisi, utadhani hakuwahi kuwa na uhusiano naye.
Nawashukuru sana wasanii wa kike wao ndiyo huungana na mimi katika maombolezo ingawa kwa mwaka huu hawakujitokeza lakini siwezi kuwasema vibaya kiukweli,” alisema mama huyo.
Nawashukuru sana wasanii wa kike wao ndiyo huungana na mimi katika maombolezo ingawa kwa mwaka huu hawakujitokeza lakini siwezi kuwasema vibaya kiukweli,” alisema mama huyo.
Baada ya habari hizi
kutoka kwa mama Kanumba, Wor’Out Media juzi lilizungumza na Ray aliyeamua
kufunguka kuwa, yeye humuenzi Kanumba kwa njia nyingi tu si lazima kujionesha
makaburini na si lazima kuutangazia umma.
No comments:
Post a Comment