Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya,Mh.Amos Makalla amepokea msaada wa mifuko 400 ya saruji,kutoka kwa
Benki ya AKIBA Commercial Bank Ltd ,kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa njia
za Wagonjwa,yenye urefu wa mita 175 katika hospitali ya Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza
hayo jana jijini Mbeya wakati wa kupokea msaada huo,RC Makalla aliwashukuru
Wadau hao kwa kujitolea na kulishughulikia ombi lake kwa haraka na kwa uzito wa
juu kabisa.
"Nawashukuru
sana Wadau AKIBA Commercial Bank Ltd , kwa kulishughulikia ombi langu
hili, ambalo sikutarajia kama lingechukua muda mfupi hivi,nawashukuru sana na
nawaomba msichoke na tuendelee kuijenga Mbeya yetu kwa
pamoja",alisema Makalla.
Makala
alisema kuwa kupitia kwa marafiki wa hospitali ya Mkoa,wanaoishi ndani na nje
ya mkoa huo,kupitia harambee walioifanya hivi karibuni wamefanikiwa kukamilisha
ujenzi wa mita 55 na na kuwa awamu ya pili inaendelea kwa ujenzi wa mita 175.
Mh.Makalla
alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya ujenzi huo,zilitumika fedha jumla ya
shilingi milioni 600,kutokana na mahitaji kuwa makubwa ya ujenzi,ujenzi
ukasimama. kwa sababu zilikuwa zikihitajika fedha nyingine kiasi cha
shilingi milioni 55,ndipo wakachukua hatua za kuomba msaada zaidi kwa wadau
ambao ni AKIBA Commercial Bank Ltd .
"Kukamilika kwa ujenzi huu kutaondoa tatizo la wagonjwa kupelekwa au
kwenda wodini kwa taabu, kwani wakati wa mvua tatizo linakuwa kubwa ",alisema
Mh Makalla.
Kwa upande wa
Akiba Commercial Bank kupitia kwa Afisa Masoko na Uendeshaji Bi Dora Saria
amesema waliguswa sana baada ya kuombwa na Mkuu wa Mkoa kutokana na wananchi
kupata shida hasa wagonjwa kwenda wodini au kupeleka maiti kwenye chumba cha
kuhifadhia maiti
Hivyo wao
kama taasisi ya Benki waliguswa na jambo hilo,na wakachukua hatua ya kuchangia
shilingi milioni 5 sawa na Mifuko 400 ya saruji na kuahidi kutoa Mafunzo na
mikopo kwa wajasiriamali
Aidha Akiba
wamevutiwa na jitihada za Mkuu wa Mkoa kuliweka jiji safi hivyo watatoa Vifaa
vya usafi na kushiriki kufanya usafi mwisho wa mwezi huu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh.Amos Makalla akikabidhiwa
mifuko 400 ya saruji na Bi. Dora Saria ambaye ni Afisa Masoko wa Akiba
Commercial Bank Jijini Mbeya.
RC Makalla akitoa neno la shukrani mbele ya Viongozi
na wafanyakazi wa Benki ya Akiba na Serikali kwa ujumla.
RC Makalla akisaidiana na Viongozi na wafanyakazi wa Benki ya Akiba na Serikali kushusha mifuko hiyo ya saruji.
No comments:
Post a Comment