Serikali kupitia
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvivu imesema imeshughulikia malalamiko ya
wakulima wa Korosho kwa kuondoa makato yasiyokuwa muhimu katika zao hilo.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri Wizara hiyo Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu hoja
mbalimbali za wabunge leo Mjini Dodoma.
“Serikali imekwisha fanyia marekebisho maeneo ambayo
wakulima walikuwa wanalalamikia kwa kuondoa kabisa makato hayo katika zao
hilo,” aliongeza Ole Nasha.
Amesema kuwa
Serikali imefuta ushuru wa shilingi 20 kwa kilo kwa ajili ya chama kikuu
cha Ushirika, Shilingi 50 za usafirishaji wa Korosho,Shilingi 10 kwa kilo
ajili ya mtunza ghala na pia shilingi 10 kwa kilo kwa ajili ya kikosi kazi
cha Masoko.Aidha Sekta ina utaratibu maalum wa kupanga bei dira kwa
kutumia vigezo vinavyokubaliwa kwa pamoja na wadau wote.
Kwa upande wa
manunuzi ya pembejeo za korosho amesema hufanywa kwa pamoja na vyombo
rasmi ndani ya Tasnia ambapo awali ilikuwa ikisimamiwa na mfuko wa
Maendeleo ya Korosho na sasa Bodi ya Korosho Tanzania.
Aidha ameeleza
changamoto zinazojitokeza katika kufikisha pembejeo hizo kwa wakulima wa korosho
na hatua zimechukuliwa kwa kushirikisha vyama vya ushirika ili kudhibiti
mianya ya pembejeo kwenda kwa wasio lengwa.
Pia Serikali
imeweka mfumo wa usambazaji wa pembejeo wenye lengo la kuhakikisha kwamba
pembejeo hizo zinawafikia walengwa pekee.
“Utaratibu huu unazingatia kutambua wakulima wenye uhitaji
na pembejeo na hununuliwa kwa kutumia utaratibu wa ununuzi wa pamoja n
akusambazwa kwa wakulima kwa kutumia wakala walioteuliwa na kudhibitishwa na
Halmashauri husika,” alisisitiza Ole Nasha.
No comments:
Post a Comment