WAUGUZI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI WASHEREHEKEA GET TOGETHER PARTY 2017 - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, April 25, 2017

WAUGUZI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI WASHEREHEKEA GET TOGETHER PARTY 2017

 Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa (wa tano kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo Dae es Salaam Jana April 22, 2017.

  Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa (wa nne kulia) akigonganisha Glas zenye kinyaji cha shampeni na Wakuu wa vitengo mbalimbali wa Hospitali hiyo
Baadhi ya Wakuu wa Idara na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa katika Gari kuelekea katika kusheherekea sherehe yao iliyofanyika Navy Beach Kigamboni Dar es Salaam jana
 Baadhi ya wanakamati wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Segla Mgaya (wa tano kushoto) ambaye ni Afisa Muuguzi wa hospitali hiyo 
 Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Agnes Mtawa  akizungumza na wauguzi hao wakati wa kusheherehekea Get Together Party 2017 iliyofanyika Dar es Salaam jana April 22, katika Ukumbi wa Navy Beach Kigamboni ambapo alipata nafasi ya kuanza kutowa salamu kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru kwakutofika. Mtawa alisema, pokeeni salamkutoka kwa mpendwa wetu Mkurugenzi, anawasalimia sana na kuwatakia heri katika sherehe hii na amesema Mungu akitupa uzima mwakani anaomba taarifa apate mapema iliaweze kuserebuka nasi na kwakumalizia salamu hizo alisema pia naomba mpoke salam zake.
 Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (kushoto) akipokea Ua kutoka kwa mtunza hazina wa Kamati hiyo, Matilda Mrina ambaye ni Afisa Mkuu Msaidizi Daraja la Kwanza. 
Meneja wa Jengo la Mwaisela, Unyanjite Hema akicheza mchezo wa karata na Muuguzi, Debora Bukuku wakati wa Sherehe hiyo.
 Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa akizindua mchezo wa mazoezi kwa kuruka kamba mbele ya Wauguzi (pichani hawapo) wakati wa kusheherehekea, Get Together Party 2017 iliyofanyika Dar es Salaam jana April 22, 2017 katika Ukumbi wa Navy Beach Kigamboni , ambapo kulikuwa na michezo mbalimbali ya kuchangamsha mwili ikiwemo, kuruka kamba, kucheza karata, kuogele, kucheza mpira na Burudani ya nyimbo mbalimbali kutoka kwa kikundi cha wasanii cha wauguzi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, michezo hiyo iliyoratibiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Segla Mgaya.
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili,(wa pili kushoto) akisindikizwa na wauguzi hao na wapilikulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Segla Mgaya.

 Muuguzi wa Hospitali hiyo, Vaileth Minja akifungua Sherehe hiyo kwa Salaa

 Wauguzi wakicheza

 Mkurugenzi Agnes Mtwa akicheza pamoja na wauguzi hao.
Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa (mwenye mkanda mweusi tumboni) akionyesha umahiri wake kwa kucheza kwaito na  wauguzi hao.

 Mwenyekiti wa Kamati hiho, Segla Mgaya akiwa katika picha ya pamoja na Wauguzi hao

Meneja wa Tawi la Benki NMB Muhimbili, (jina halikupatikana mara moja) akizungumza na wauguzi hao akisisitiza, anaomba kushirikiana na Wauguzi hao, hayo aliyasema wakati wa Sherehe ya ‘Get Together Party 2017’, iliyofanyika Dar es Salaam jana katika Ukumbi wa Navy Beach Kigamboni, alianza kwa kusema, 

“Sisi wana wa NMB tunaamini kwa wafanyakazi wanapokutana kwa pamoja wanaongeza ufanisi wa kazi kwa sababu wanakutana pamoja na wanapokuwa Muhimbili kila mmoja anakuwa Bize na kazi yake, lakini hapa mnaweza kubadilisha mawili matatu nakuweza kubadilisha mawazo”,

Aliendelea  kusema “Sisi wana wa NMB tunaimani wafanyakazi wa Muhimbili wana watoto, kwahiyo tumewaletea bidhaa adimu ya mototo Akaunti ambayo unaweza kuifungua pale kwetu katika Tawi letu lililopo Muhimbili”, alisema.

Ninaimani pale kwetu tunavibanda kama sita ambavyo kuna wahudumu na ukifika pale utamwambia muhudum unahitaji huduma hiyo na atakuletea fom na utaijaza na kingine siolazima kwa wewe kuja Benk kuja kuweka pesa.

Utajazishwa fomu ambayo ikifika tarehe ambayo uliambia benk utakumbushwa na ile pesa itatoka kwenye Akaun yako na itakwenda kwenye Akaut Mtoto. alisema Menena huyo.

Huduma hiyo nimbure kabisa kwani kwakufanya hivyo nikuwaandalia watoto wetu msingi bora wa maisha na kuwaandalia ufanisi wao katika masomo yao ya kila siku.

Karibuni sana na ninaomba tuendelee kushirikiana asanteni sana .
 Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa akiwaonyesha zawadi aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Segla Mgaya (wa kwanza kulia) iliyo andaliwa wauguzi hao.

 Afisa Muuguzi, Agnes Kaberege akifungua Shampeni.

 Wauguzi wakicheza

Mkurugenzi wa Uuguzi akiwasalimia wauguzi na kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa kuwepo mahala hapa kwa siku ya leo.

Mtawa alisema, nijambo la kihistaria mimi tangu niingie kufanya kazi hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili sikumbuki kufanya kitu kama hiki.

Kwakweli nawashukuru kwa kubuni wazo kama hili na kwa sisi tuliyofika hapa na ninajuwa wauguzi tupo wengi lakini niwachache walioitikia wito na ninafikiri huu ni mwanzo mzuri.

Mungu akitupa Uzima wakati mwingine hapa patakuwa hapana nafasi ya kucheza pamoja na mvua nyingi lakini mmeweza kujitowa kwa kuja mahali hapa, alisema Mtawa.

Nawaomba nduguzangu Wauguzi tuendelee kuwa na umoja kwa kushikamana kama tulivyoonyesha siku ya leo, tuendelee kupendana, kupeana nguvu kwa sababu kazi yetu kama mnavyo ijuwa kunachangamoto nyingi.

Lakini tukiwa kama mahala kama hapa tunacheza na kufurahi ausio jamani? kwa kuangalia Bahari na yale mabo mengine mengine tumeyaacha getini, kwahiyo pamoja na shukrani nyingi nawaomba tufurahi kwa pamona, alisema Mtawa kwa kumalizia.

Leo si siku ya hutuba ni siku ya kufurahi 

 Wauguzi wakicheza




 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Segla Mgaya (kulia) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Agnes Mtawa, wanaoshuhudia ni wanakamati
 Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (wa nne kulia) walio kaa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Sherehe hiyo
 Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (wa tatu kulia) walio kaa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benk ya NMB


 Wauguzi wakicheza
 Wauguzi wakicheza
 Wauguzi wakicheza
 Wauguzi wakiwa katika picha za pozi
Wauguzi wakiwa katika picha za pozi

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages