Tamasha la muziki la MTN BUSHFIRE 2017 rasmi kufanyika Mei 26-28 Nchini Swaziland - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, April 25, 2017

Tamasha la muziki la MTN BUSHFIRE 2017 rasmi kufanyika Mei 26-28 Nchini Swaziland


Tayari tamasha kubwa la Muziki linalofanyika kila mwaka  mwezi Mei, nchini Swazland linalojulikana kama  MTN Bushfire limezinduliwa rasmi wiki iliyopita huku kwa sasa likisubiriwa kwa hamu kufanyika hiyo Mei 26-28. 2017,nchini humo.

Tamasha hilo ambalo kila mwaka linakuwa ni la kuvutia na lenye mvuto wa aina  yake, ni miongoni mwa matamasha makubwa Barani Afrika ambalo upaswi kurikosa kabisana tayari tiketi za za tamasha hilo zimeanza kuuzwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa mtandao (Online)

Kwa mwaka huu mbali na jukwaa kuu, pia kutakuwa na jukwaa maalum la “MTN Bushfire Firefly STAGE”, kwa udhamini wa MTN, ambapo itakuwa ni maalum kutoa nafasi kwa wasanii chipukizi na wa ndani ya Swaziland ambao watapata kuonesha vipaji vyao.

“Jukwaa hili litajumusha wasanii wa vikundi zaidi ya 100 ambao ni wa ndani pekee na wataonesha ushindani wao  na  Mei 5,2017, vikundi vitatu ambavyo vimefanya vizuri vitachaguliwa kushiriki MTN Bushfire 2017” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa wasanii wapya watakaopamba jukwaa hilo kwa mwaka huu ambao tayari wametangazwa ni pamoja na: Zahara, Mozambiques The Mute Band, Aero Manyelo, Spoek Mathambo’s Batuk Collective, American acapella group.

Wengine ni Hugh Masekela, Tkzee, Jah Prayzah, GoodLuck, Jermemy Loops, Faada Freddy, The Kiffness, Matthew Mole, Baloji, Bombino, Jojo Abbot na wengine wengi.

Kwa upande wa Madjs ni pamoja na DJ Fred Spider (France), Karla Kenya (Swaziland/Germany/USA), Itallo Dlamini (Swaziland),  Vukazithathe (South Africa), Easy Freak (South Africa) Bholoja (Swaziland) , Hanwah (UK), Dusty & Stones (Swaziland), Lodanda (Swaziland), Nicholas Ellenbogen’s Theatre for Africa (South Africa).


No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages