Serikali imesema jumla ya
walimu 3,081 wakiwemo walimu 7 wa shule ya Sekondari Omumwani Kagera,
wameajiriwa, hivyo bado kuna nafasi ya walimu 1.048 kati ya nafasi 4,129 za
walimu wa Sayansi na Hisabati zilizotolewa kibali cha ajira.
Taarifa hiyo imetolewa
leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akizungumza na Waandishi
Habari, ofsini kwake ambapo amewataka walimu wote walioajiriwa wanatakiwa
kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 18 hadi 25 mwezi huu.
Amesema walimu
walioajiriwa wamepangwa moja kwa moja na TAMISEMI katika halmashauri zote
nchini ambazo zina upugufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati.
Simbachawene amesema kati
ya walimu hao walioajairiwa walimu 1,537 ni wa Shahada na walimu 1,544 ni
wa Stashahada.
“Sehemu kubwa ya walimu
wa Shahada wamepangwa kwenye shule za kidato cha tano na sita na wachache
kwenye shule za kidato cha kwanza hadi cha nne’’ alisema.
Simbachawene
amekiri kuwa kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo Sayansi na Hisabati
katika shule mbalimbali za sekondari nchini.
“Moja ya changamoto kubwa
ambazo zinaikabili sekta ndogo ya elimu ya sekondari ni upungufu wa walimu wa
Sayansi na Hisabati upungufu uliopo katika shule 3,602 ni 26,026 sawa na
asilimia 60.14 ya walimu 43,248 wanaohitajika” amesema Simbachawene
Amesema walimu
wanaohitajika kwa masomo hayo ni walimu 43,248 lakini waliopo kwa sasa ni
17,252 pekee.
Amesema kwa sasa serikali
ina shule za sekondari 3,602 na kati ya hizo shule 333 ni za kidato cha tano na
sita huku zingine 54 za kidato cha tano zimeanzishwa .
Aidha amesema shule hizo
za sekondari kwa upande wa masomo ya Sanaa ina ziada ya walimu 7,463 ambapo
waliopo ni walimu 63,240 na wanaohitajika ni walimu 55,777.
“Kutokana na ziada hiyo
ya walimu wa Sanaa serikali imeanza kuchukua hatua yawahamisha walimu hao
katika shule za msingi ili kuziba upungufu wa walimu katika shule hizo’’ alisema.
No comments:
Post a Comment