Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Scrabble - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, April 13, 2017

Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Scrabble


Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mashindano  ya mchezo wa Scrabble (pichani) yanayotarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia Aprili 14 hadi 16,2017 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa mashindano ya Scrabble, Nicholas Mbugua amesema mashindano hayo yatashirikisha wachezaji 80 kutoka Kenya, Uganda, na Afrika Kusini.

Katika hatua nyingine, Chama cha Wachezaji Scrabble nchini (TASPA) kimeahidi kuufufua mchezo huo hasa katika vyuo vikuu na shule za msingi na sekondari.

Katibu wa TASPA, Toyo Kitua wakati akizungumza na waandishi wa habari, Aprili 10,2017 jijini Dar es Salaam amesema awali walijaribu kuufufua mchezo huo ila walikwama kutokana na ukosefu wa fedha.

“Mara ya kwanza tuliuanzisha lakini tulikwama sababu ya ukosefu wa fedha ila hivi sasa tunataka kuufufua hasa kwenye shule na vyuo nchini. Mchezo huu ni mzuri kwa wanafunzi sababu ni mgumu unaohitaji kutumia akili,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages