Thursday, April 13, 2017

SERIKALI KUDHIBITI BIASHARA YA VYUMA CHAKAVU
Serikali kupitia Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa Rasimu ya Muswada wa Sheria itakayoweka bayana taratibu na mfumo wa
usimamizi na udhibiti wa bishara ya
chuma chakavu katika hatua mbalimbali za uzalishaji, ukusanyaji, usambazaji,
uuzaji na uyeyushaji wake kwa kuzingatia uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa manufaa ya Taifa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
Biashara ya Chuma chakavu
imeshamiri hapa nchini na duniani kwa ujumla na hili limetokana na mahitaji ya vyuma chakavu ambapo kumetumiwa na
wahalifu kuaharibu miundombinu
iliyojengwa kwa vyuma kwa nia ya kupata chuma ili waiuze kama chuma chakavuâ€Alisema Mwijage.
Amesema ili kukabiliana na
hujuma hizi Mamlaka husika zikiwemo TANESCO, TANROADS na RAHACO wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na jeshi la
Polisi ikiwemo kutumia walinzi wa
Taasisi husika ili kulinda rasilimali hizo.
Amesisitiza kuwa Muswada
huu umeweka wazi na bayana adhabu itakayotolewa kwa mtu atakayebainika kuharibu miundombinu.
Aidha Mhe.Mwijage ametoa
wito kwa watanzania kutoa taarifa pindi waonapo mtu anayehujumu miundombinu kwa namna yote ile.
“Natoa wito kwa wenye
viwanda na wafanyabiashara wa vyuma chakavu
jiepusheni na ununuzi wa vyuma ambavyo asili yake ina mashaka
na tutaharakisha sheria hii ili kutatua tatizo hili,” aliongeza Mwijage.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya Scrabble
Older Article
YANGA KUONDOKA NA MSAFARA WA WACHEZAJI 20 LEO, CHIRWA ABAKI
TAASISI ZA UMMA NA SEKTA BINAFSI SHIRIKIANENI - WAZIRI KOMBO
Hassani MakeroFeb 27, 2025SERIKALI KUJENGA KIWANDA KIKUBWA CHA SUKARI
Hassani MakeroFeb 26, 2025MSAJILI WA HAZINA NA CAG KUSHIRIKIANA KATIKA USIMAMIZI WA MASHIRIKA YA UMMA
Hassani MakeroFeb 26, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment