Katibu Mkuu wa Yanga
Chrles Mkwasa
Kelekea mechi ya
marudiano ya mchezo wa hatua ya mtoano wa Kombe la Shirikisho baina ya
wawakilishi wa Tanzania klabu ya soka ya Yanga na
Mc Alger ya Algeria imeweka wazi kikosi cha wachezaji 20 watakaoondoka leo
kuelekea nchini Algeria jioni.
Yanga wanatarajiwa kuondoka
jioni majira ya saa 12 kuelekea nchini Algeria ambapo watacheza na MC Alger
siku ya Jumamosi katika Jiji la Alger.
Akiweka kikosi hicho,
Katibu Mkuu wa Yanga Chrles Mkwasa amesema kuwa tayari wachezaji wapo tayari
kwa ajili ya kwenda kupambana nchini Algeria na tunafahamu ni mchezso mgumu lakini
pia ni muhimu sana kwao wakihitaji ushindi wa aina yoyote au sare ili kusonga
mbele na kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Mkwasa amesema kuwa
anapenda kuwa msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka
leo jioni majira ya saa 12 kwa ndege ya shirika la Emirate kupitia Dubai.
Wachezaji watakaondoka ni
Makipa; Deogratius Munishi na Beno Kakolanya. Nafasi ya ulinzi ni ; Nadir
Haroub, Vicent Bossou, Juma Abdul, Vicent Andrew, Oscar Joshua, Juma Abdul,
Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani.
Nafasi ya viungo ni;
Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke, Said Makapu, Juma Mahadhi,
Saimoni Msuva, Geofrey Mwashuiya na Emmanuel Martin.
Upande wa washambuliaji
ni Amissi Tambwe na Donald Ngoma
Wachezaji wafuatao
wataukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali Justine Zulu, Malimi Busungu, Matheo
Antony, Ally Mustapha, Pato Ngonyani, Obrey Chirwa na Yusuph Mhilu.
No comments:
Post a Comment