KIKOSI cha timu ya Simba
kimeendelea kujifua kwa nguvu wakijiandaa na mchezo wa nusu fainali dhidi ya
Azam utakaofanyika mwishioni mwa wiki hii.
Jumamosi ya April 29, ni
nusu fainali ya kwanza ya kombe la Shirikisho la Azam HD baina ya Simba na Azam
itakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Kwa sasa Simba wapo
Morogoro wakijiandaa na mchezo huo ambapo chini ya Kocha Joseph Omog na Jackson
Mayanja kimeamua kujichimbia huko kwa ajili ya kuwapa muda wa kupumzika
wachezaji wake na kuwapa mbinu mpya mbalimbali.
Hii inakuwa ni mechi ya
ushindani mkubwa sana kwa timu hizi mbili zikikutana kwa mara ya tatu ndani ya
msimu mmoja ambapo katika michezo miwili ya awali ila mmoja akishinda mchezo
mmoja.
Kwa mujibu wa Kiongozi wa
Simba, Abbas Ally amesema kuwa wachezaji wana ari kubwa sana na wako vizuri na
wanaamini watapigana mpaka mwisho ili kupata ushindi kwenye mchezo huo.
"Huu ni mchezo
muhimu sana kwetu, ni muhimu kupata ushindi ili tuweze kuingia fainali ya
kombe la Shirikisho na wachezaji wana ari kubwa sana ya ushindi na wameahidi
kupambana mpaka mwisho,"amesema Ally.
Mpaka sasa Kikosi cha
Simba kinakabiliwa na majeruhi wawili ambao wanatarajiwa kuukosa mcheoz huo
ambao ni Hamad Juma na Jamal Mnyate.
Wachezaji wa Simba wakiwa katika mazoezi ya pamoja kulekekea mchezo wao
wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi dhidi ya
Azam.
Golikipa Peter Manyika akiwa katika mazoezi kulekekea mchezo
wao wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi dhidi ya
Azam.
Wachezaji wa Simba wakimsikiliza Kocha Joseph Omog katika maandalizi ya
mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi.
Wachezaji
wa Simba wakiwa katika mazoezi ya pamoja kulekekea mchezo wao wa nusu
fainali ya kombe la Shirikisho la Azam HD siku ya Jumamosi dhidi ya Azam.
No comments:
Post a Comment