Balozi wa Tanzania nchini
Uingereza, Dkt. Asha Rose Migiro leo aliandaa hafla fupi katika makazi ya
Balozi kumpongeza kijana mtanzania Alphonse Simbu Kwa kushika nafasi ya tano
katika mbio za "London Marathon" zilizofanyika tarehe 23 Aprili 2017
jijijini London.
Katika salamu zake,
Balozi Migiro alimpongeza Bw. Simbu kwa heshima aliyoipa Tanzania jijini London
na Duniani kupitia mbio za London. alimsihi atumie matokeo hayo kama
hamasa ya kufanya bidii zaidi kwa ajili ya mashindano ya mbio ndefu
anayotarajiwa kushiriki baadae mwakani.
Simbu alimshukuru Balozi
Migiro Kwa ushirikiano mkubwa wa kibalozi alioupata akiwa jijini
London. Alimkabidhi Balozi Fulana ya kumbukumbu ya ushiriki wake kwenye mbio
hizo.
No comments:
Post a Comment