Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya
Trilioni 10.87 mpaka kufikia Machi mwaka huu kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo
Charles Edward Kichere wakati wa mahojiano na mtangazaji wa TBC1 Rashid Salum
katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa kila siku za Jumatatu saa moja
kamili jioni na Alhamisi saa tatu na nusu usiku.
Kichere alisema, mwaka huu wa fedha 2016/2017 TRA
inatakiwa kukusanya Trilioni 15.105 na hadi kufikia Machi mwaka huu TRA
imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 10.87.
Aliendelea kwa kusema kuwa mpaka kufikia Juni mwaka
huu TRA itahakikisha inatimiza lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 15.105 ili
kusaidia Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake.
Alisema kuwa TRA ina waajiriwa wapya ambao wamepewa
mafuzo ya miezi sita katika chuo cha kodi juu ya mifumo mbalimbali ya
ukusanyaji kodi ambao waliajiriwa moja kwa moja na mamlaka hiyo kwaajili ya
kutekeleza majukumu ya ukusanyaji kodi ndani ya nchi.
“Tunatumia mfumo wa Tehama kukusanya kodi na mifumo
mingine mbalimbasli kama vile Tigo Pesa , Airtel Money na MPesa ili
kurahisishia watu kulipa kodi wakiwa nyumbani na kuepuka usumbufu,” alisema
Kichere.
Kichere aliongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha mapato yameongezeka mpaka kufikia asilimia 9.9 hadi 10 licha ya kuwa kuna baadhi ya maeneo hawakuweza kukusanya.
Kichere aliongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha mapato yameongezeka mpaka kufikia asilimia 9.9 hadi 10 licha ya kuwa kuna baadhi ya maeneo hawakuweza kukusanya.
Aidha Kichere alisema Mamlaka kwa sasa imejipanga
kuwa na mahusiano mazuri na wafanyabiashara ili kuhakikisha wafanyabiashara wanalipa
kodi stahiki na kwa mujibu wa sheria bila kutumia nguvu au uonevu wowote.
Hata hivyo mamlaka hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa
walipa kodi kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kutoa semina kwa
watumishi wa umma , kuandaa makongamano ambayo yanatoa elimu, kupitia mitandao
ya kijamii na ziara mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya ili kuhakikisha
wafanyabiashara wanapata elimu pamoja na kujua wajibu wao katika kulipa kodi
ili kuleat maendeleo nchini.
No comments:
Post a Comment