Ujumbe wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN)
Tanzania, ukiongozwa na Mratibu wa Mashirika hayo, Mh. Alvaro Rodriguez
umetembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa lengo la kujuwa maendeleo yake.
Wajumbe wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania wakitembelea wodi
mpya ya wazazi ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Mhandisi Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja Bi Mathna Kassim Marine akitoa
maelezo kwa Mratibu wa Mashirika ya UN alipotembelea sehemu ya kuzalisha gesi
ya Oxygen inayotumika katika Hospitali hiyo.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania Alvaro Rodriguez
akiuliza swali kwa uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja alipotembelea Hospitali
hiyo kujuwa maendeleo yake.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Naufal Kassim Mohd akitoa
maendeleo na changamoto za Hospitali ya Mnazimmoja wakati Ujumbe wa Mashirika
ya UN ulipotembelea Hospitali hiyo.
Ujumbe wa Mashirika ya UN Tanzania ukiongozwa na Alvaro Rodriguez wa
kwanza (kushoto) ukitembelea Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
No comments:
Post a Comment