Wanafunzi wa shule ya
Msingi Ushindi iliyopo mikocheni B jijini Dar es salaam, Wamepatiwa mafunzo
maalum ya elimu ya Usalama barabarani na jeshi la polisi la Usalama barabarani
kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania PLC.
Elimu hiyo imetolewa leo
ikiwa ni mwendelezo wa jeshi hilo na Vodacom Tanzania kutoa elimu hiyo nchi
nzima,Wanafunzi walipata fursa ya kujifunza alama muhimu za barabarani na
matumizi ya barabara na mambo muhimu ya kuzingatia kuwaepushia ajali wanapokuwa
wanatumia barabara wakati wa kwenda na kutoka shuleni na matembezi mengineyo.
Akiongea kuhusiana na
mafunzo ya elimu hiyo ya Usalama barabarani Afisa mnadhimu kutoka makao makuu
ya jeshi hilo SSP, Tabita Makaranga ameipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga
mkono jitihada za serikali katika
kutokomeza ajali za barabarani “Kwa kutoa elimu hii kwa
watoto wadogo waliopo mashuleni kwa
kiasi kikubwa tutaweza kupunguza tatizo hili kwa kuwa wataendelea kukua wakijua
matumizi sahihi ya barabarani na kwa upande wao ni rahisi kuelewa kuliko watu
wazima.
Siku hii imekuwa muhimu
kwa wanafunzi hawa kwani maisha yao yapo mikononi mwetu kwani ajali za
barabarani zimekuwa ni janga la kitaifa na duniani kote ambapo taasisi
mbalimbali zinazohusika na kupambana na ajali zinaendelea kulipigia kelele kwa
Nguvu zote“Ni wakati wa kukumbuka
sasa –Sema Hapana kufanya uhalifu wa
barabarani”.Alisema Makaranga
Naye Mkuu wa Mkuu wa
kitengo cha Usalama barabarani na mahala pakazi wa Vodacom Tanzania PLC,Karen
Lwakatare amesema kuwa suala la kuelimisha jamii kuhusiana na usalama
barabarani ni jambo ambalo kampuni ya
Vodacom itaendelea kulivalia njuga kwa nguvu zote kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi na wadau wengine.
“Tatizo la ajali nchini ni
kubwa na kila mwaka wananchi wengi hupoteza maisha kutokana na ajali za
barabarani ikiwemo idadi kubwa ya watu kubaki wakiwa na ulemavu wa aina
mbalimbali pia ajali zinaathiri familia nyingi kutokana na wategemezi katika
familia kupoteza maisha ama kupata ulemavu kutokana na ajali hususani za
barabarani”.
Alisema tatizo hili ili
kulitokomeza linahitaji ushirikiano wa watu wote “Vodacom tumekuja na
mikakati mbalimbali ya kufanya kampeni hizi mojawapo ikiwa kupeleka elimu ya
usalama barabarani kwa watoto wadogo waliopo mashuleni kama tulivyofanya leo na
mkakati huu unaendelea kutekelezwa katika mikoa mbalimbali”.Alisema.
Lwakatare alisema mbali
na elimu mashuleni Vodacom kwa kushirikiana na serikali kupitia Jeshi la Polisi
na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani imekuwa ikiendesha kampeni ya “Wait to Send” ambayo inahamasisha madereva wanaoendesha
vyombo vya moto kutotumia simu za mkononi wanapokuwa barabarani na kutotumia
vinywaji vyenye kilevi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto kwa ajili ya
kulinda usalama wao,abiria wanaowabeba na watumiaji wengine wa barabara.
Mwanafunzi wa shule ya msingi
Ushindi Mikocheni B jijini Dar es Salaam, Issa Abdallah (kushoto) akiwasomea
wanafunzi wenzake bango lenye ujumbe wa Usalama barabarani wakati wa mafunzo
maalum ya elimu ya Usalama barabarani yaliyoendeshwa na Jeshi la polisi la
Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania PLC.
Mwanafunzi wa shule ya msingi
Ushindi Mikocheni B jijini Dar es Salaam,Emanuel Andrea (kulia) akiwasomea
wanafunzi wenzake bango lenye ujumbe wa Usalama barabarani wakati wa elimu ya
mafunzo maalum ya Usalama barabarani yaliyoendeshwa na Jeshi la polisi la
Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania PLC.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya
msingi Ushindi Mikocheni B jijini Dar es Salaam pamoja na Mkuu wa kitengo cha
Usalama barabarani na mahala pakazi wa Vodacom Tanzania PLC,Karen Lwakatare(wakwanza
katikati)wakimsikiliza Askari wa Jeshi la Usalama barabarani CPL,Faustina
Ndunguru(kulia) akiwafundisha alama za barabarani wakati wa mafunzo maalum ya
kuvuka barabara kwa wanafunzi hao yaliyoendejeshwa na jeshi hilo kwa
kushirikiana Vodacom Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment