Katibu Mtendaji wa Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kununua hisa kwenye
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Serikali
imewataka watanzania kuchangamkia fursa ya ununuzi wa asilimia 25 ya hisa za
awali za kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom zinazouzwa kwa watanzania pekee
ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2016 kwa lengo la kuwawezesha
watanzania kuwa wamiliki makampuni ya simu za mikononi hapa nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi Beng’i Issa amesema hi ni fursa kubwa na
muhimu kwa watanzania kuwa sehemu ya wamiliki wa makampuni ya simu za mikononi
kupitia ununuzi wa hisa hizi za awali.
‘’Ni
uwekezaji ambao ni salama sana na hauna hasara, kwa kuwa ukiwa hutaki kuendelea
kuwa mwanahisa unauza hisa zako na kurudisha pesa zako na unaweza kupata
faida’’.
Ununuzi wa
hisa hizi utawawezesha Watanzania kuwa wamiliki wa kampuni, watapata gawio la
faida, wanaweza kutumia hisa kama dhamana za mikopo benki na wanaweza kuziuza
hisa wanapokuwa na shida ya fedha.
Hisa hizi
zinauzwa kwa mtanzania mmoja mmoja, watumishi walioajiriwa, wastaafu, makampuni
yanayomilikiwa na watanzania, mashirika ya kitanzania, VICOBA, SACCOS, vikundi
vya kijamii, wanawake na vijana. Aidha hisa moja inauzwa kwa shilling 850 na
kiwango cha chini cha ununuzi ni hisa 100 na hakuna kikomo cha juu cha ununuzi
wa hisa.
Baraza
linatoa rai kwa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii Nchini, Taasisi za fedha, Vikundi
vya fedha vya kijamii kuwezesha wanachama na wateja wao kununua hisa hizi za
awali.
Ununuzi wa
Hisa hizi unapatikana kupitia matawi ya benki ya NBC, NMB, CRDB nchi nzima,
mawakala wa soko la Hisa la Dar es Salaam, M-PESA na matawi mbali mbali ya
benki za biashara nchini.
Baraza
linawahamasisha watanzania wote kuchangamkia fursa hii muhimu ili kushiriki
kikamilifu katika kumiliki uchumi wao na kufikia ndoto ya kuwa Taifa la uchumi
wa kati kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Mwaka 2025.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa
kununua hisa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango mkoani Dodoma.
Afisa Mawasiliano
Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bw. Edward
Kessy, akitoa ufafanuzi wa namna ya kununua hisa hizo kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango mkoani Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa
habari wakifatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’I Issa (hayupo pichani) alipokuwa
anatolea ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kununua hisa kwenye mkutano uliofanyika
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa
habari wakifatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’I Issa (hayupo pichani) alipokuwa
anatolea ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kununua hisa kwenye mkutano uliofanyika
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment