UBALOZI WA KOREA WASAIDIA KUKAMILISHA AHADI ZA SERIKALI YA MKOA WA DAR ES SALAAM KWA KUJENGA HOSPITALI YA KISASA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, April 13, 2017

UBALOZI WA KOREA WASAIDIA KUKAMILISHA AHADI ZA SERIKALI YA MKOA WA DAR ES SALAAM KWA KUJENGA HOSPITALI YA KISASA


Katika kutimizwa kile kinachoitwa Deni la serikali ya Mkoa kwa wakazi wake wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda leo hii ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Kinamama ya Chanika unaofadhiliwa na ubalozi wa Korea Kusini na kugharimu zaidi ya Tshs. 8.8 Bilioni za kitanzania uliokamilika  kwa 90% hadi hivi sasa.

Ujenzi huo ambao ulizinduliwa kwa kuwekewa jiwe la msingi  na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda mwishoni mwa mwaka jana baada ya ombi la ujenzi wa Hospitali ya kisasa kwa wamama na mtoto wakazi wa Dar es salaam kupokelewa na kukubaliwa na ubalozi wa Korea kusini hapa nchini.

Ukamilishwaji wa ujenzi huu unasindikizwa pia na ujenzi wa nyumba 28 za makazi kwa ajili ya wauguzi na madaktari watakaohudumu hospitali hiyo masaa 24.

Ukamilishwaji wa ujenzi huu ambao hadi sasa umebakiza hatua ya mwisho ya ufungaji wa vitanda 160 vya wagonjwa na 10 vya kujifungulia wakina mama wajawazito  (ambayo ni 10% ya mradi wote), ni uthibitisho tosha wa kuonesha nia ya dhati ya Serikali ya Dr John Pombe Magufuli ya kuhakikisha huduma bora za kiafya zinawafikia wananchi wote wa Tanzania kwa wakati.

Hospitali hii ya kihistoria na aina yake itakuwa ni mahusisi kwa wakina mama wa Mkoa wa Dar es salaam na wamama wote wa maeneo jirani na inatarajiwa kufunguliwa mwezi Juni mwaka huu (2017) na Mh rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dr.John Pombe Magufuli.

Akiongea katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema, “Kwa ukamilifu wa Hospitali hii tunategemea kupungua vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua, na kuwa jambo la bahati mbaya na si ukosefu wa vifaa.”

Pongezi nyingi zimfikie Mh Paul Makonda kwa jitihada za kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Dar es salaam kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo hapa nchini.

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda alipotembelea hospitali hiyo iliyopo Wilaya ya Ilala, Chanika KOICA, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
 Mmoja wa maafisa wa manispaa ya Ilala akimpokea Mkuu wa Mkoa alipotembelea hospitalini hapo.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dkt. Willy Sangu akionyesha ramani ya jengo la hospitali ya Mama na Mtoto, kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda alipotembelea hospitali hiyo iliyopo Chanika KOICA, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bi Grace Magambe akifafanua jambo juu ya uwezo na ubora wa kifaa tiba kilichofungwa mahala hapo katika hospitali hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda alipotembelea hospitali hiyo iliyopo Wilaya ya Ilala, Chanika KOICA, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda, akitaka maelekezo ya matumizi ya moja ya vifaa tiba kutoka kwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dkt. Willy Sangu wa pili (kushoto), alipotembelea Hospitali ya mama na mtoto iliyopo Wilaya ya Ilala, Chanika KOICA, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bi Grace Magambe na watatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mh Sophia Mjema.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akifanya uchunguzi jinsi kifaa hicho  
 kinavyoweza kufanya kazi katika hospitali ya mama na mototo alipotembelea hospitalini hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akitoa maelezo kwa waandishi wa habari jinsi Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe Magufuli ilivyokusudia kutatua kero za wananchi katika sekta ya afya akionesha moja ya kifaa tiba cha kisasa kilichopo katika hospitali hiyo alipokwenda kutembelea hospitali ya mama na mtoto iliyopo Wilaya ya Ilala, Chanika KOICA, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, ambayo ipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi ambao umekamilika kwa asilimia 90.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bi Grace Magambe akifafanua jambo juu ya uwezo na ubora wa huduma itakayotolewa katika hospitali hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda alipotembelea hospitali hiyo iliyopo Wilaya ya Ilala, Chanika KOICA, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 

 Moja ya vifaa tiba vilivyopo katika hospitali hiyo
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema, akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akikagua moja ya vitanda vya kisasa vya wagonjwa vilivyopo katika hospitali hiyo.
 Vitanda vya kisasa vya wagonjwa vilivyopo katika hospitali hiyo.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dkt. Willy Sangu akielezea jambo kwa Mkuu wa Mkoa
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bi Grace Magambe akifafanua jambo juu ya uwezo na ubora wa vifaa vilivyopo katika hospitali hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda alipotembelea hospitali hiyo iliyopo Wilaya ya Ilala, Chanika KOICA, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema (kushoto), akielezea jinsi vifaa hivyo vya kisasa vitakavyoweza kuwasaidia wakina mama ambao watakwenda kupata huduma ya matibabu katika hospitali hiyo pia amewataka wakina mama wote wa Dar es Salaam kwenda kupata huduma hospitalini hapo kwani imejengwa mahususi kwaajili yao, ameyasema hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda alipotembelea hospitali hiyo iliyopo Wilaya ya Ilala, Chanika KOICA, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akipitia kitabu cha maelekezo cha moja ya vifaa tiba vilivyopo hospitalini hapo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akitoa maelezo ya kina kwa waandishi (hawapo pichani) kuhusu vifaa vilivyopo hospitalini hapo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akijifunza jambo kivitendo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda walipotembelea hospitali hiyo iliyopo Wilaya ya Ilala, Chanika KOICA, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Moja ya vifaa tiba vilivyopo katika hospitali hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akipata maelezo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bi Grace Magambe wa pili (kushoto)  juu ya matumizi ya mashine ya kufulia ambayo ina uwezo wa kufua nguo zenye ujazo wa kg 70 kwa mkupuo mmoja, mashine hiyo ipo kwaajili ya kutoa huduma kwa  wakina mama ambao watakwenda kujifungua au kupata huduma katika hospitali hiyo, iliyopo Wilaya ya Ilala, Chanika KOICA, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Moja ya majengo ya malazi kwa Wauguzi watakaokuwa wakifanyakazi hospitalini hapo
  Moja ya vifaa tiba vilivyopo katika hospitali hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda akifanya majaribio ya kifaa tiba kimoja wapo alipotembelea hospitali ya mama na mtoto iliyopo Wilaya ya Ilala, Chanika KOICA, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages