Afisa Uhusiano wa Airtel
Tanzania, Jane Matinde (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Mwenyekiti
wa Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma, jijini Dar es Salaam jana, kwa
ajili ya kusadia timu ya taifa ya wanawake ya Kilimanjaro Queens, ili
kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya
nchini. Kulia ni Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sebastian Nkomwa na Nahodha, Sophia
Mwasikili.
Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel leo imetoa vifaa vya michezo kwa timu ya taifa ya wanawake ya
Kilimanjaro Queen kwa lengo la kuiwezesha timu hiyo kuwa na vifaa bora
vitakavyowawezesha kuendelea kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na
nje ya nchi.
Vifaa hivyo ambavyo ni
pamoja na viatu vya mpira pair 20 na socks pair 40 vitawawezesha wachezaji hao
kuondoka na changamoto ya vifaa vya michezo hususani viatu bora vya kuchezea
mpira ambavyo ni nyenzo muhimi katika mchezo wa soka.
Akiongea baada ya
kukabidhiwa vifaa hivyo kwa niaba ya timu ya Kilimanjaro Queens, Mwenyekiti wa
soka la wnawake Amina Karuma alisema “ Tunajisikia furaha kupokea vifaa hivi na
nawapongeza sana Airtel kwa kutimiza ahadi yao yakutupatia vifaa lakini pia kwa
kuunga mkono jitihada za kukuza soka la wanawake nchini. Airtel imekuwa mstari
wa mbele katika kuchochea kukua kwa soka la wanawake kwa kushirikisha timu za
wasichana katika michuano ya Airtel Rising Stars kila mwaka na kwa kupitia
michuano hii tumeweza kupata vipaji tunavyoviona leo katika timu zetu za
wanawake.
“Tunawahakikishia vifaa
hivi vitatusaidia saana kwani viatu vya mpira ni nyenzo muhimu sana lakini pia
ni moja kati ya changamoto kubwa kwa wachezaji wetu. Tunayo mipango mingi na
michuano mbalimbali iliyopo mbele yetu na tumejipanga kufanya vizuri lakini pia
kujiandaa vyema kwa michuano ya AFCON inayotegemea kuanza Februari Mwakani.
“Aliongeza Karuma.
Kwa upande wake Afisa
Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema “ katika kuhakikisha tunaendeleza
kukuza soka la wanawake nchini tumeona ni vyema kuwapatia wachezaji wa timu ya
taifa ya Kilimanjaro Queen vifaa hivi ili kuwapa motisha ya kuendelea kufanya
vizuri zaidi lakini pia kutekeleza adhima yetu ya kukuza mpira wa wanawake
nchi. Tunapenda kuwapongeza sana Kili Queen kwa kufanya vizuri katika
mashindano mbalimbali ikiwemo michuano ya CECAFA ambapo timu hii iliibuka kuwa
washindi na hivyo Airtel kuahidi kuwapatia vifaa ili kuendelea kuboresha
kiwango chao cha mpira”.
Tunajisikia furaha
kutimiza ahadi hii na ni matumaini yetu vifaa hivi vitatumika vyema kwenye
michuano mingi ijayo katika mwaka huu pia. Aliongeza Matinde.
Kikosi cha Kilimanjaro
Queens kinajengwa na wachezaji 8 walioibuliwa kutoka katika michuano yakukuza
vipaji vya mpira kwa vijana ya Airtel Rising Stars yanayodhaminiwa na
kuendeshwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kila Mwaka.
No comments:
Post a Comment