Kamanda wa Polisi Kanda
maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na tukio la uvamizi wa Mkutano wa wanachama wa CUF uliotokea mwishoni
mwa wiki hii.
Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watano kwa tuhuma za
kushiriki tukio la uvamizi wa Mkutano wa wanachama wa CUF uliofanyika Vinna
Hotel Mabibo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kamanda wa
Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema hayo leo wakati
akiongea na waandishi wa Habari jijini hapa. Amesema kuwa. Aprili 22 mwaka huu
majira ya mchana, walipokea taarifa ya kuwa watu wasiofahamika wakiwa na silaha
walivamia mkutano huo na kujeruhi baadhi ya watu.
Kamanda Sirro
ameongeza kuwa, mpaka sasa watuhumiwa watatu waliokamatwa wanaendelea kuhojiwa
na upelelezi utakapokamilika hatua za kisheria zitafuatwa juu yao na amewasihi
watu kutii sheria bila shuruti kwani hakuna mtu au kikundi chochote cha watu
wanaoweza kuwa na mamlaka ya kushambulia wengine.
"Kama
unamalalamiko pitia polisi, au mahakamani siyo kuvamia kundi la watu wengine
kama wako juu ya sheria, tunafuatilia wale wote waliohusika katika kufanya
shambulio hilo na mtu mmoja aliyejeruhiwa sana anataja watu walioshambulia"
amesema Sirro.
Kamanda
Sirro, amesema jeshi la polisi linaamini kuwa watu waliofanya uvamizi huo
walifanya kwa utashi wao wenyewe na kwamba pindi upelelezi ukikamilika
watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani.
Aidha amewaonya
baadhi ya viongozi wa CUF waliotangaza kuwafuata watu fulani na kuwawajibisha
ni vema wakumbuke kuwa hakuna mtu aliyeko juu ya sheria kwani hakuna mtu
aliyeko juu ya mamlaka.
Mapema wiki
iliyopita, watu wasiojulikana wakiwa na bastola walivamia mkutano wa wanachama
wa CUF ambao wanamuunga mkono, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na
kuwapiga wanachama wa CUF pamoja na waandishi wa habari ambao walikuwepo eneo
hilo.
Mkutano huo
ambao ulikuwa na lengo la kumtambulisha Katibu Mkuu wa CUF, ulivurugika baada
ya vurugu kubwa zinazodaiwa kufanywa na wanachama wa CUF ambao wanamuunga mkono
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
Katika vurugu
hizo, Mtu mmoja ambaye bado hajafahamika jina lake miongoni mwa waliovamia
mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu
kutoroka.
No comments:
Post a Comment