Mkurugenzi
Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt, Fadhil Mohd Abdalla akimkaribisha Naibu
Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman kuzungumza na waandishi wa habari katika
maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika ukumbi wa Wizara ya Afya
Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Naibu
Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akizunguza na waandishi wa
habari katika maadhimisho ya siku ya Malaria Dunia katika ukumibi wa mikutano
wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Mwandishi
wa habari wa ITV/Radio One Farouk Karim akiuliza swali katika maadhimisho hayo
yaliyofanyika kwa mkutano wa waandishi wa habari katika Wizara ya Afya
Mnazimmoja.
Meneja
Kitengo cha Kumaliza Malaria Zanzibar Mwinyi Issa Khamis akijibu maswali ya
waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya malaria yaliyoadhimishwa kwa
mkutano wa waandishi wa habari Wizara ya Afya Zanzibar .Picha na Makame
Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman amesema
pamoja na mafanikio makubwa katika kupambana na Malari Zanzibar, bado shehia
tano zinaendelea kutoa wagonjwa wa maradhi hayo zaidi ya asilimia tano.
Akizungumza na waandishi wa habari katika
maadhimisho ya siku ya Malaria Dunia katika ukumibi wa mikutano wa Wizara ya
Afya Mnazimmoja, amezitaja shehia hizo kuwa ni Tumbatu Jongowe, Miwani, Micheweni,
Chukwani na Kiwengwa.
Hata hivyo amesema maambukizi ya malaria katika
maeneo hayo yanasababishwa na wasafiri wanaoingia na kutoaka nje ya Zanzibar
mara kwa mara ambapo mwaka jana asilimia 55 ya wagonjwa waliogundulika walikuwa
na tabia hiyo.
Amesema takwimu za Malaria Zanzibar zinaonyesha
mafanikio mazuri ambapo mtu mmoja kati ya watu mia moja hupata ugonjwa huo
katika jamii isipokuwa shehia hizo tano.
Naibu Waziri wa Afya amewataka wananchi kuendelea
kuchukua tahadhari za kujikinga na Malaria ikiwemo kutumia vyandarua
vilivyotiwa dawa na kusafisha mazingira kwa lengo la kuondosha mazalio ya mbu
wanaoeneza maradhi hayo.
Ameongeza kuwa Serikali kwa upande wake mwaka jana
iligawa vyandarua 705,000 bila malipo na kufanya zoezi la kupiga dawa nyumba za
wananchi ya kukinga malaria bila ya kuangalia vyeo vya wamiliki wa nyumba hizo
licha ya kukabiliana na changamo nyingi katika kazi hiyo.
Amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakikataa
kupigiwa dawa nyumba zao kwa madai kwamba zinawaletea athari za afya jambo
ambalo halina ukweli kwani dawa hiyo ni salama kwa afya.
Amekubusha kuwa Sheria ya Afya ya Jamii na
Mazingira ya mwaka 2012 pamoja na mambo mengine inasisitiza juu ya udhibiti wa
mbu na mazingira hivyo wananchi watakaokataa kupigiwa dawa sheria itawabana.
“Watu wanaokataa nyumba zao kupigiwa dawa ya
kukinga maluaria bila sababu za msingi zinazokubalika, sheria hii itawabana na
hatua muafaka zitachukuliwa dhidi yao,” alisisitiza Naibu Waziri.
Meneaja Kitengo cha kumaliza malaria Mwinyi Khamis
alisema Zanzibar imeweka mikakati ya kumaliza kabisa malaria ifikapo mwaka 2023
hivyo juhudi za jamii na Wizara ya Afya ni muhimu.
Amesema mwaka jana watu watano walibainika kufa kwa
malaria Zanzibar wakiwemo watoto wawili wenye umri chini ya miaka mitano.
Mapema akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi
wa Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Mohd amewashauri wananchi wasikubali kula
dawa ya malaraia bila kupimwa na kuthibitishwa kuwa wanayo malaria.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inasema Malaria bado ipo Zanzibar, chukua tahadhari.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inasema Malaria bado ipo Zanzibar, chukua tahadhari.
No comments:
Post a Comment