Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki
ya NMB, Richard Makungwa (kulia), akimkabidhi Katibu wa Timu ya Singida United,
Abdurahman Sima, mipira na vifaa vingine vya michezo vyenye thamani ya
sh,milioni 10 Dar es Salaam leo kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara itakayoanza Agosti mwaka huu.
Katibu wa Timu ya Singida United, Abdurahman Sima
(kushoto), akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea vifaa hivyo.
Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki
ya NMB, Richard Makungwa (katikati), akizungumza katika hafla ya kukabidhi
vifaa hivyo. Kulia ni Mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuph Mwandani.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Hapa ni makabidhiano ya jezi.
Vifaa vilivyokabidhiwa vikioneshwa kwa wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki
ya NMB, Richard Makungwa (katikati), akisisitiza jambo baada ya kukabidhi
msaada huo.
BENKI ya NMB imetoa
msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10 kwa timu ya
Singida United kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
itakayoendelea kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada huo makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo, Ofisa
Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Richard Makungwa alisema msaada huo
umelenga kusaidia timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa kwa ligi hiyo.
"Tumetoa msaada huu
kwa timu ya Singida United kwa kwa ajili ya maandalizi ya ligi hiyo na hii ni
kawaida yetu kusaidia timu mbalimbali pale tunapopata nafasi" alisema
Makungwa.
Makungwa alisema licha ya
benki hiyo kufanya shughuli za kibenki pia imejikita kuinua michezo nchini kwa
kutoa msaada wa vifaa vya michezo.
Alitaja vifaa walivyotoa
msaada kwa timu hiyo ni viatu vya mpira wa miguu, jezi na mipira vyote vikiwa
na thamani ya sh.milioni 10.
Katibu wa timu hiyo
Abdurahman Sima alisema vifaa hivyo walivyopata vitatumika kwa lengo
lililokusudiwa na si vinginevyo.
"Tunaishukuru benki
ya NMB kwa msaada huu tunaomba wadau wengine kuiga mfano wa benki hii "
alisema Sima.
No comments:
Post a Comment