China imepiga hatua nyingine katika
mpango wake wa anga za juu, baada ya kuanza kufanyia majaribio mpango wa
kupeleka binadamu wakaishi kwa muda mrefu kwenye Mwezi.
Wanafunzi wa sayansi wamehamia katika
chumba maalum chenye mazingira yanayofanana na ya Mwezi ambapo watakaa kwa siku
200.
Lengo ni kuwaanda kwa safari ya kuishi
kwa muda mrefu kwenye kituo cha anga za juu kwenye Mwezi, bila kupokea usaidizi
wowote kutoka ardhini.
China imewekeza pesa nyingi sana katika
mpango wake wa anga za juu, ikilenga kushindana na Marekani na urusi.

No comments:
Post a Comment