Monday, May 15, 2017

BOT yaifungia benki ya jamii ya Mbinga
Benki Kuu ya Tanzania
imeamua kuifunga Mbinga Community Bank Plc, kusitisha shughuli zake zote za
kibenki na kufuta leseni yake ya biashara ya kibenki kuanzia tarehe 12 Mei,
2016.
Aidha Benki Kuu ya
Tanzania imeiweka Mbinga Community Bank Plc chini ya ufilisi na kuiteua Bodi ya
Bima ya Amana kama mfilisi kuanzia tarehe 12 Mei, 2017, kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Benki Kuu leo asubuhi imeeleza.
Uamuzi huu umechukuliwa
baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa Mbinga Community Bank Plc ina
upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki an
Taasisi za Fedha ya wmaka 2006 na kanuni zake.
“Upungufu huu wa mtaji na
ukwasi unahatarisha usalama wa sekta ya fedha, na kwamba kuendelea kwake kutoa
huduma za kibenki kunahatarisha usalama wa amana za wateja,” taarifa hiyo
imeeleza.
Aidha, Benki Kuu ya
Tanzania imeuhakikishia umma kuwa “itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana
katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.”
Benki Kuu ya Tanzania
imechukua uamuzi wa kuifunga benki hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 56(1) (g),
56(2) (a), (b) na (d), 58(2) (i), 11(3) (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya
Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.
Tags
# BIASHARA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Nicki Minaj akanusha kuwa mpenzi wa rapa Nas….
Older Article
CHINA YAPELEKA BINADAMU KUISHI MUDA MREFU MWEZINI
ABSA YAZINDUA MKOPO MPYA WA MALI ZA KIBIASHARA,SERIKALI YAPONGEZA JITIHADA
Hassani MakeroApr 04, 2025AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAPELEKA TABASABU KITUO CHA KULELEA WATOTO CHAKUWAMA
kilole mzeeMar 28, 2025Taasisi za Ulinzi wa Mlaji zimetakiwa kushirikiana na FCC
Hassani MakeroMar 21, 2025
Labels:
BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment